Habari

Darassa: Mtaa unaniinspire kuandika ngoma zangu

Rapper anayehit na ngoma ‘Nishike Mkono’, Darassa amesema nyimbo zake nyingi huziandika kutokana na mambo yanayotokea mtaani anakoishi ambako watu wengi hawana maisha mazuri.

Bongo5 ilipiga story na Darassa katika show ya After School Bash iliyofanyika Jumamosi iliyopita pale Mbalamwezi Beach ambako naye aliperform na kumuuliza kwanini nyimbo zake zinahusu maisha ya tabu zaidi.

“Mimi niko mtaani na kuna vitu vyote hivi, maisha yetu sisi yako huko tunafanya kwaajili ya watu wa mtaani. Mtaani kuna mambo mengi na kati ya vitu ambavyo viko mtaani hakuna good times. Hakuna good life hiyo ambayo labda kuna watu wengine wanaishi,”alisema Darassa.

“Kwahiyo mimi najaribu kuandika maisha halisi ambayo nakutana nayo mtaani na watu wa karibu ambao naishi nao, pengine inaweza kuwa sio mimi tu kwasababu mimi siwezi kuwa na shida kila siku, najaribu kuangalia maisha ya watu wengi nayafanyia nyimbo na vitu kama hivyo.”

Darassa amesema mwaka 2013 anakuja na project mpya na amesema atautumia kufidia machungu aliyoyapata wakati akihangaika kutoka kimuziki. Pia Darasa anatarajia kutoa filamu yake iitwayo Sikati Tamaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents