Burudani

Darassa aweka wazi mpango wa kuachia albamu

Hit maker wa wimbo ‘Muziki’ Darassa amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya albamu yake mpya.

Rapper huyo amedai hatua hiyo itawafanya mashabiki wa muziki wake kupata nyimbo zake nyingi kwa pamoja.

“Tutakuwa na albamu mwaka huu ambayo itarahisisha watu kupata muziki wote wanaouhitaji, tupo kwenye kipindi cha mabadiliko na nafanya ninachoweza kwa watu wangu,” Darassa alikiambia kipindi cha 3600 cha EFM.

Katika hatua ngingine rapper huyo amezungumzia kauli za baadhi ya wasanii wa hip hip ambao wanadai hawajaelewa alishokifanya kwenye wimbo Muziki.

“Na deal na mtu ambae yupo tayari kupokea muziki wangu sitakuwa na comment kwa atakaenipinga. Changamoto zinanijenga badala ya kufikiria kitu chako ukanifikiria mimi kwenye kitu chako maana yake nimekuchallenge,” alisema Darassa.

Wimbo huo wa Darassa bado unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio huku katika mtandao wa YouTube ikikaribia kufikisha views milioni 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents