Habari

Darassa akanusha kutumia unga, asema kuna watu wamepanga kumchafua

Rapper Darassa amekanusha kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kudai kuwa kuna watu wake wa karibu walioamua kumchafua ili kumpoteza kwenye game.

10522436_835817866479952_2471091865650333714_n

Darassa ameiambia Bongo5 kuwa, hajutii kwa lililotokea kwani atajifunza kutambua nani anafaa kuwa rafiki wa kweli kwenye maisha yake.

“Ni kitu ambacho mtu anataka kuHaribu kitu cha mtu, watu wengi wananitegemea mimi na nipo na heshima zangu na nipo hivyo,” amesema Darassa.

“Kuna watu wananijua wanataka kuona mimi napotea kwenye kiwango. Kwenye sehemu ambayo hawataki mimi niwe kwaajili ya kuwafelisha watu wanaonipenda. Kwahiyo watu ambao wame-create hivyo vitu ni watu wangu wa karibu na wametengeneza hivyo baada ya mimi kuchagua kuachana nao na kuamua kutafuta rafiki wengine ambao wanaweza kunishauri mimi nini cha kufanya.”

“Kwahiyo ilifikia stage ya kuachana na marafiki wa mwanzo ambao walitengeneza hivyo vitu. Sijutii hiki kilichotokea na sijawahi fanya hivyo. Ninachoweza kusema ni kwamba wamejaribu kunizushia natumia madawa lakini mimi ninachowaambia sijatetereka na sijutii kwa hili lililojitokeza, nitasonga mbele na kufanya mambo mazuri zaidi.”

Hivi karibuni Darassa aliachia ngoma mpya iitwayo ‘Tunaishi’ aliyomshirikisha Nay wa Mitego.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents