Burudani

Darassa afunguka kuhusu kutajwa kama rapper namba 1 na mashabiki

Rapper anayefanya vizuri kwa sasa kwenye muziki wa Hip Hop, Darassa amefunguka juu ya mtazamo wa mashabiki na wadau mbalimbali kumtaja kama ndio rapper namba moja kwa sasa nchini.

15101783_554164378116470_9052220755500072960_n

Darassa amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, “Sikuwa nimeplan hivyo lakini naona watu wanaweka huo mtazamo kwa sasa kutokana na hard work niliyoionyesha na still nipo bado nipo kwenye changamoto ya kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha nafikia malengo yangu. Lengo langu si kuamka asubuhi watu wakasema mimi ndio best rapper au mimi ninaweza kuwa mkali kwenye hiki kipindi lengo langu ni kuweka historia kwenye muziki wangu hata kama nisipotoa wimbo historia yangu ibaki inafanya kazi. Naomba Mungu anisaidie sana kwa hili.”

“Nafikiri Too Much inahitaji wimbo mwingine kwa sababu toka nimeutoa hakuna wimbo mwingine unaweza kukaa juu ya wimbo huo. So hakuna sababu ya sisi kuendelea kusubiri mashabiki wetu wanahitaji burudani, ndio sababu kubwa imepelekea kuleta project hii mpya.”

Rapper huyo ameongeza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Muziki’ ambao mpaka sasa umetazamwa zaidi ya mara 801k kwenye mtandao wa Youtube umetayarishwa na maproducer watatu akiwemo Mr VS, Mr T-Touch na Abbah wa Abbah Process.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents