Darasa la Kili Music Awards
Washiriki waliopendekezwa kuwania tuzo katika shindano la Kili Music
Awards mwaka 2009, majuzi walipewa somo juu na namna ambavyo mashindano
hayo yatakavyoendeshwa kwa mwaka huu.
Akizungumza katika semina iliyowahusisha wasanii hao na wadau mbalimbali wa muziki, Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndiyo wadhamini wa mtanange huo Oscar Shelukindo, amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwajuza washiriki namna ambavyo mashindano hayo yataendeshwa kwa mwaka huu pamoja na masuala yanayohusiana na mchakato mzima wa Tuzo za muziki
Katika Semina hiyo Shelukindo amesema kuwa wameshirikiana na wawakilishi kutoka BASATA pamoja na COSOTA ili kuweza kuboresha mchakato mzima wa TUZO hizo.
Shelukindo amesema katika siku ya kuwatangaza washindi pale Diamond Jubilee, wasanii mbalimbali watapanda na kutumbuiza ukumbini huku akitumia fursa nyingine kuwataja wasanii hao kuwa ni pamoja na Nameless (Kenya), Blue 3 (Uganda) huku Tanzania iiwakilishwa na TID, Keysha, African Stars, Twanga Pepeta, Barnabas, Wakali kwanza pamoja na AY.
Bofya hapa kuangalia mahojiano na video za wasanii wengi kutoka seminar iliyofanyika majuzi.