Habari

Dar Kupata Umeme Mdogo

Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, watakuwa wanapata huduma ya umeme mdogo kwa nyakati za mchana kutokana na mnara mmoja unaoendesha umeme kuharibiwa

Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, watakuwa wanapata huduma ya umeme mdogo kwa nyakati za mchana kutokana na mnara mmoja unaoendesha umeme kuharibiwa.

 
Mnara huo wenye nambari 324 wenye uwezo wa Kv 220 unaotokea mkoani Morogoro hadi kufikia jijini Dar es Salaam, umeharibiwa watu wasiofahamika wakati walipokuwa wakiiba nyaya kwenye mnara huo juzi usiku.

 
Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), iliyotolewa jana, ilisema kutokana na laini ya pili ya mnara huo kufanya kazi, hakutakuwa na giza Dar es Salaam isipokuwa kutakuwa na kupungua kwa umeme kwa nyakati za mchana.

 

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema wahandisi wa shirika hilo wameshaanza kazi ya kurejesha hali kama ilivyokuwa kawaida lakini hawajasema kuwa shughuli hiyo itamalizika kwa muda gani.

 
Kutokana na wizi huo polisi kwa kushirikiana na uongozi wa Tanesco Mkoa wa Morogoro wanawatafuta watu waliohusika na wizi huo na wameahidi hatua kali za kisheria zitachkuliwa ili iwe mfano kwa wezi wengin ambao wamepelekea kitendi hicho kukithiri katika sehemu mbali mbali hapa nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents