Habari

Daladala kuanza kutoa tiketi za kielektroniki kwa abiria wao

Serikali inaendelea kuboresha vyanzo vyake vya mapato ili kukusanya kodi ipasavyo ambapo imepanga kuanzia mwakani nauli zote za mabasi yanayotoa huduma za usafirishaji abiria mijini maarufu kama daladala kutoa risiti za kielektroniki kwa abiria wao.

daladala

Imesema lengo la mpango huo ni ili kubaini kipato halisi cha wamiliki wa mabasi hayo na kuimarisha ukusanyaji kodi.

Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na nchi Kavu SUMATRA Bw. Johansen Kahatano wakati wa uzinduzi wa kamapeni ya uvaaji sare kwa madereva daladala nchini.

Amesema kuwa zoezi hilo liko katika hatua za ukamilishaji na kuanzia mwezi wa kwanza mwakani mfumo huo utaanza kutumika lengo likiwa kuboresha na kubadilisha uhusiano baina ya mmiliki na mfanyakazi wa gari.

Amesema malipo hayo yatasaidia serikali kufikia lengo lake la kuifanya ajira ya udereva kuwa rasmi kama kazi nyingine kwa kuwa mapato yote yatakuwa yanaonekana serikalini na kuwabana wamiliki wa magari kutoa ajira za mikataba kwa wafanyakazi wao.

Sambamba na hilo serikali imetoa muda wa wiki mbili kwa wamiliki wa daladala kununua sare za wafanyakazi wao na kwa wale watakaokiuka maagizo hayo watafutiwa leseni zao.

Kwa upande wa madereva kwa kupitia Mwenyekiti wao Bw. Shabani Mdemu amesema wamekubaliana na maagizo hayo kwakuwa lengo lao ni kwamba serikali ihalalishe kazi ya udereva ili wapate haki zao za msingi hasa malipo yao ya msingi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents