Burudani

Cyrill Kamikaze aeleza kwanini ngoma zake hazifanyi vizuri, azitaka media ubadilika (Video)

Rapper Cyrill Kamikaze amefunguka na kueleza vikwazo mbalimbali ambavyo vimekwamisha baadhi ya ngoma zake kushindwa kufanya vizuri.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, rapper huyo kwa upande wake mwenyewe ameitupia lawama management yake kwa kushindwa kumfikisha sehemu ambayo alikuwa anaitaka.

“Mimi nilikuwa na management tulitofautiana kidogo kwa sababu ilikuwa haijakaa vizuri kidogo, ukizingatia mimi niko busy kidogo, mimi ni mfanyabiashara, mambo mengi nafanya mimi, kwa hiyo ziwezi kufanya kila kitu peke yangu,” alisema Cyrill.

Aliongeza, “Kwa mfano mimi naenda kufanya interview lakini management ina deal na muziki wangu, mimi binafsi siwezi kufanya kila kitu, kwa management kwa mwaka jana haijafanya vizuri sana lakini mwaka huu nitaishape,”

Kuhusu ngoma zake nyingi kutofanya vizuri mwaka jana rapper huyo amezitupia lawama media.

“Media zijikumbushe nyuma tulikuwa na akina Juma Nature, Ngwea na wasanii wengine na kila mtu alikuwa anapewa nafasi, ningependa kushauri kwamba watangazaji na Djs japo siyo wote watoe nafasi kwa wasanii wote, ushabiki uwe wa mtu binafsi siyo wa media, kila mtu apewe nafasi halafu majaji wawe mashabiki, ukiwa wewe mtangazaji ndio jaji kwa sababu una power, unampenda fulani, ukiingia kwenye uteam, ndio mambo kama haya yanajitokeza,” alisema Cyrill.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents