Michezo

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa Ureno

Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ureno mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika usiku wa March 21, mjini Lisbon,Ureno. Amewashinda Pepe na kipa Rui Patricio katika kinyang’anyiro hicho.

Cristiano Ronaldo ambaye ana miaka 32, alichukua ubingwa wa UCL na Real Madrid mwaka jana kabla ya kuiongoza Ureno kuchukua ubingwa wa michuano ya Mataifa Ulaya nchini Ufaransa.

Hii ni mara ya 8 Ronaldo kuchukua tuzo hiyo.
Washindi wengine ni Renato Sanches wa Bayern Munich ambaye amechukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi na Kocha wa timu ya Taifa ya Ureno Fernando Santos akichukua tuzo ya kocha Bora wa Mwaka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents