Burudani

Crazy GK aelezea mamilioni ya shilingi yalivyopukutika kutengeneza video yake mpya

Video ya wimbo mpya wa Crazy GK ‘Mzuri Pesa’ imetoboa mifuko yake kwa kiasi kikubwa, kwa mujibu wa yeye mwenyewe.

50c05dcc-c322-4f75-b495-0cb7e902da5b

Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, rapper huyo aliyegeuka muimbaji, amedai kuwa alilazimika kuwasafirisha waongozaji wawili wa nje, mmoja wa Uganda na mwingine wa Afrika Kusini kwaajili ya kazi hiyo.

Amedai kuwa pamoja na gharama za kuifanya video hiyo, alilazimika kuwalipia gharama za hoteli kwa takriban wiki mbili.

Kingine amesema ni nguo zilizotumika kwakuwa alimpa kazi mbunifu wa mitindo kutengeneza nguo za wote wanaoonekana humo. Lengo la kufanya hivyo anasema ni kutengeneza brand yake kwa kutoa kitu bora.

Sikiliza zaidi interview hiyo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents