Burudani

Cpwaa asema muziki ni mgumu ila muda ndio huu, Prof J adai atafanya ‘maamuzi magumu’

Ni kama vile muziki unanufaisha wasanii wachache mno nchini. Tukianza kuwataja wasanii wanaoweza kujitokeza na kusema wazi kuwa muziki unawapa fedha nyingi, hawewezi kuvuka 20, wachache wanapata za kawaida sana na wengi mambo ni magumu. Na ni kweli hali halisi ni kuwa wasanii wengi wanalalamika kuwa muziki ni mgumu kuliko kawaida.

cpwaa3

Hata hivyo hilo si jambo linalomuumiza kichwa rapper wa Chereko Chereko, Ilunga Khalifa aka Cpwaa kwakuwa anaamini muziki wa Tanzania bado upo kwenye hatua ya ‘makuzi’.

“Music Industry ya Tanzania bado iko kwenye “growing phase” things are not balanced yet because of matatizo fulani sugu ambayo mwisho wake unakuja kutokana na mabadiliko ya teknolojia na matumizi yake,” ameandika Cpwaa kwenye Facebook.

“Kama nchi nyingine na kama sector zingine za kibiashara tutapitia hizi phases mpaka vitu vitakaa sawa.Muziki umekuwa mgumu na ndio unalipa zaidi hii ni moja ya changamoto na mafanikio yake.Wale ambao wameanza hii safari siku nyingi,msikate tamaa huu ndio muda wa kujipanga upya na kucapitalize. Kama we ni mfanya biashara unayependa kuinvest in long term business,the time is now! Ngoma bado mbichi hii,anza leo ‪#‎ThinkTank‬.”

Kwa upande wa Profesa J aliyeguswa na kauli hiyo ya Cpwaa, mwaka 2014 kwake ni mwaka wa kujitoa muhanga.

“Mwaka huu lazima tufanye maamuzi magumu maana this is too much. … ENOUGH is ENOUGH,” amesisitiza Profesa.
Unazungumziaje kauli za mastaa hao? Unahisi kwanini muziki umekuwa mgumu na kwanini ni wasanii wachache tu wananufaika na muziki? Nini cha kufanya?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents