Burudani

Cpwaa afunguka kuhusiana na kasoro za biashara ya muziki wa Tanzania, ‘wasanii wengi wamekata tamaa’

Ilunga Khalifa aka Cpwaa ameamua kufunguka kwa kina kuhusiana na kasoro kubwa zilizopo kwenye biashara ya muziki wa Tanzania ambazo zimefanya wasanii wachache tu ndio wanufaike nao.

Cpwaa

Hivi ndivyo alivyoandika:

Let me take this off my chest before my new releases:

Mzunguko wa hela kwenye industry ya muziki umekua mdogo Tanzania kutokana na upendeleo na kipaumbele kupewa wasanii wachache.Vipaumbele hivi ni kwenye shows pamoja na airtime redioni.Hii inachangia sana kushuka kwa input ya content kutoka kwa wasanii wengi.Wanaopendelewa ni aidha wanastahili au kwa sababu ya faida za watu fulani binafsi wenye interest zao,ambapo kiukweli kwenye ushindani wa biashara hatuwezi kuwalaumu.Je na wale wasio na kitu inakuaje?

Wasanii wengi na baadhi ya maproducers wamepunguza kasi ya kutoa nyimbo kwa sababu ya tatizo hili, hivyo kuamishia creativity yao kusaka pesa kwa njia zingine.Ujumbe wangu kwa wadau wote: Jitahidini sana kustick kwenye basic procedures,kama mtu akikupa sawa lakini ni jukumu lenu kuhakikisha jamii inapata ladha tofauti hata kama kuna watu wanashinikiza aina fulani tu ya muziki kwa misingi ya biashara.Sasa hivi wasanii wachanga hawaumizi vichwa kwenye concepts na mashairi! sababu wanajua ishu ni hela tu nikiwa nayo natoka! namiss zamani ambapo ukisikia flani anatoa nyimbo unaisubiri kwa hamu na unaitafuta.

Siku hizi hatuwasikii hata wakitoa nyimbo na wakitoa hazidumu.Na wasikilizaji nao washazoe “spoon feeding” chochote tu wao twende! Tunahitaji diversity and creativity virudi kwenye muziki wetu ili Cash flow iongezeke, show ziwe nyingi,mauzo ya album yarudi,wasanii wapate hela ya kuendesha muziki wao na maisha yao ili gurudumu zima lisogee in general.Sababu hao mnaowabeba saa hivi wakishuka nani atawapa hizo pesa nyingi mnazotaka?

Jifunzeni kubalance the market sio mnabanabana tu! Wasanii wengi wako demoralized wengine wamekata tamaa, wengine mpaka wanakimbilia Kenya.Kwa nini mnaua soko lenu? Tanzania should have been the biggest threat,and multi-billion dollars entertainment Industry in Africa kushinda Afrika magharibi na kusini tukicombine na Fashion,sports,and Films! Demographically and Statistically we deserve that!!.

Kila msanii akipata haki yake ndio mabilioni yataingia kutokana na faida,TRA wapatapa chao,COSOTA watapata chao,Wasanii watapata hela ya studio,video na promotion na nyie pia mtapata chenu badala ya kupokea mtonyo kwa wawili utapokea kwa watu 20! It is simple mathematics you morons, japo hairusiwi na haikubaliki. Think Tank! Msiue vipaji for no reason sasa kwa mfano sasa hivi tunasikiliza nini? Main stream is full of crap! hamna jipya!

Before the Internet comes and kill your business anzeni kubadilika na kuplay your role in empowering artists kama mnataka mzidi kupata pesa.Mfano mzuri ni wahindi…Nani anahangaika na Mamu siku hizi? The Tradtional Music distribution business is dying .Mtazamo wangu tu na inamhusu mdau yeyote ambae yupo kwenye mziki bila kuchagua wala kubagua ( iwe Media,Kampuni za simu,Entertainment Companies,Agencies,Managers,Artists na affiliated parties). The Consiousness is real!!! and is progressing!! #PowerOfTheInternet #SlowCancer #PwaaaSaid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents