Sat 13 Mar 2010
Sasa habari zinapatikana kwa kiingereza na kiswahili, chagua lugha upendayo hapo juu
Henry Joseph rasmi Norway E-mail
Henry Joseph rasmi Norway
Kiungo mkabaji wa Simba na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Henry Joseph Shindika, jana alisaini mkataba wa miaka minne kusakata soka ya kulipwa katika klabu ya Kongsvinger ya Norway

Kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo, Mehdi Remtulla, Henry alisaini mkataba kuichezea klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, ambayo ilianzishwa mwaka 1892.

“Kwa sasa timu hiyo ya Kongsvinger inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ya Daraja la Kwanza inayoshirikisha timu 16, ambapo mwishoni mwa msimu, timu mbili zitapanda na kushiriki Ligi Kuu ya Norway,” alisema Remtulla.

Kwa mujibu wa Remtulla, Henry amefurahishwa na kufikia makubaliano ya kucheza soka Ulaya, na kuahidi kujituma ili kufungua njia kwa nyota wengine wa Tanzania kufikia hatua hiyo au zaidi.

Habari zinasema, chini ya mkataba huo nyota huyo atakuwa akilipwa fungu nono, ikilinganishwa na viwango vya nchini Tanzania, ingawa halikuwekwa bayana.

Aidha, Tanzania imepanda kwa nafasi 12 kwa ubora wa soka duniani kwa mujibu wa viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ikitoka nafasi ya 109 hadi 97, huku Brazil ikirejea nafasi ya kwanza kutoka ya tano.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage, kwa Afrika, Tanzania sasa inakamata nafasi ya 23, huku ikiwa ya tatu kwa Afrika Mashariki na Kati, nyuma ya Uganda na Sudan.
Aidha, Misri ambao ni vinara wa Afrika, wao wanakamata nafasi ya 38 kimataifa, wakifuatiwa na Algeria ambayo kimataifa ni ya 47, huku Tunisia ikiwa ya 49.

Akizungumzia mafanikio hayo, Kocha Mkuu wa Stars, Mbrazil Marcio Maximo alisema ni faraja kubwa na kusema hayo ni matokeo ya juhudi ya pamoja wachezaji, benchi la ufundi, TFF , wadhamini na wapenzi kwa ujumla.

Maximo alisema, juhudi hizo ndizo zimewafanya wachezaji wa Tanzania waanze kupata soko kimataifa kama kiungo wa Moro United, Nizar Khalfan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Comments (9)Add Comment
...
written by a guest, July 03, 2009 - 03:28:35
Kazi mzuri kijana, mpira wetu usiishie Bongo tu, laziwe tuwe na impact on international level. Ndugu kacheze boli, tunakutakia kila la heri.
...
written by a guest, July 04, 2009 - 04:43:27
hongera mazee nenda kawakilishe Tzee majuu, kumbuka huu ni mwanzo tu bado unasafari ndefu kaka, kajitume ili uwafungulie njia na wengine.
big up.
Katema, wa Mnarani Beach.
...
written by a guest, July 05, 2009 - 21:51:55
nenda kacheze mpira hachana majungu hapa nyumbani kwani mafanikio yako ndio yawanasimba pamoja na tanzania kwa jumla mungu ibariki tanzania na ubariki maisha marefu kijana huyu
Baba shani zanzibar
...
written by a guest, July 08, 2009 - 00:38:36
karibu hapa norway wabongo wenzio tupo wengi hapa tutaksapoti kimtindo kaza boot mwana hiyo ndiyo mofano tunatakiwa kuionyesha dunia kuwa hata wabongo tunaweza. hongera shindika.
...
written by a guest, July 09, 2009 - 21:18:41
emwana piga kazi, koku ale
...
written by a guest, July 10, 2009 - 13:58:58
mshikaji nenda ukajitume uwasaidie wanamichezo wengine wa tanzania jitume sana mafanikio ndio yameanza ila ushauri wangu kwako kaka use you tallent to rich the succesfull.Marino from ARUSHA.
...
written by a guest, July 11, 2009 - 07:48:50
Hongera mwana Henry Joseph Shindika kwa mafanikio yaliyoanza kujitokeza. Watanzania wote tupo nyuma yako. By Kambi Mbwana.
...
written by a guest, August 07, 2009 - 16:08:12
henry mwana komaa kwani wao wameweza wana nini? huna mpinzani kwenye kiungo.
...
written by a guest, November 11, 2009 - 07:52:49
safi sana Henry Joseph, nyota nilianza kuiona tangu kwenye umiseta.
Aah mimi kaka yako augustino kalumuna nimeacha mpira si unajua umri tena .Ila kama Maximo angekuja bongo mapema labda ningekuwa Man utd.
Big up

Write comment
quote
bold
italicize
underline
strike
url
image
quote
quote
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley
Smiley

busy
Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 

Who's been doing what

13 March, 2010
profile update, 12:52
chumamoto updated their profile photo.

new user registration, 07:11
chumamoto joined our community! Welcome!

new user registration, 06:53
tashu joined our community! Welcome!

profile update, 00:30
MTU PORI updated their profile photo.

12 March, 2010
new user registration, 18:39
a78saa joined our community! Welcome!

profile update, 16:59
helenaa updated their profile photo.

status update, 16:21
mycle Am juc chln' waitn' 4 dinner

new user registration, 14:29
markone joined our community! Welcome!

new user registration, 13:52
semhando joined our community! Welcome!

new user registration, 13:33
servasadolph joined our community! Welcome!

The Weather

Dar es Salaam, , TZ

Now
Partly Cloudy
32°C, Windchill: 32°C
Wind: 27 kph N
Humidity: 65%
Visibility: 0 km
Preasure: 1,005 mb steady
Sunrise: 6:28 am
Sunset: 6:37 pm
Sat
Sunny
Hi: 33°C, Low: 27°C
Sun
Partly Cloudy
Hi: 33°C, Low: 27°C

Sudoku

othman shouts:
Gaucho nimekumiza nini kaka?nasikitishwa sana na muafrica wewe kunita mie ni mtu mmbaya sana !!naka

Latest Members Pics

 

Latest Songs

Not a Flirt
K-Lynn ft Hermy B
Ulinikuta
Klex ft Stone
Chupa Nyingine
Mchizi Mox
Shikide
Dully Sykes
Nimetoka Mbali
Jaguar ft. AY

Latest Videos

We have 83 guests online and 2 members online
4pak100 golgotha
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
total 25713 registered
female 6293 female
male 19307 male
month 45 new this month
New: chumamoto