SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Kila la Kheri Amanda PDF Print E-mail
Friday, 04 July 2008

amanda_2.jpg

 

Watanzania tumeweza kumpata Miss Universe Tanzania Bi Amanda Sululu ambaye amemrithi Mwanadada Flaviana Matata aliyewahi kubahatika kufikia mpaka hatua ya kumi bora katika mashindano kama hayo yaliyowahi fanyika mwaka jana.

Kuchaguliwa kwake kuwa Miss Universe Tanzania kunampa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Universe kinachotarajiwa kufanyika huko Vietnam mnamo July 14 ambapo washiriki zaidi ya 80 kutoka kote duniani wanatarajiwa kuwepo katika kuwania taji hilo.

Kutoka Afrika walioingia hatua hiyo ni Tansey Coetzee kutoka Afrika ya Kusini na warembo kutoka Misri, Ghana, Mauritius na Nigeria hawapo katika orodha hiyo.

Miss Universe Venezuela, Diana Mendoza ameshika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo akifuatiwa na warembo wa Marekani, Puerto Rico, Panama, Trinidad and Tobago, Mexico, Ireland, Australia, Colombia na Thailand.

Kwa namna moja au nyingine hii ni hatua mojawapo ambayo inaipatia sifa nchi yetu pamoja na kuitangaza kwa ujumla…hatuna jinsi zaidi ya kumtakia kila la kheri Mtanzania mwenzetu Amanda Sululu.

 

 amanda_1.jpg

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
Flavour - Hongera Mamaa!! Fri, 04th Jul 08 - 11:26 am
Nafikiri ni nafasi nzuri tu ya kuitangaza Tanzania kwa jinsi hii.Kila raia wa Tanzania anajitahidi kwa uwezo wake ni jinsi gani atatoka ili nae aitangaze nchi yake.Ulipofikia mamaa ni paziru kaza buti usonge mbele tunakutakia kila la heri bint!!!
Nisipitwe - Best wishes. Fri, 04th Jul 08 - 10:01 pm
Miss wetu tunakutakia kheri inshallah.kaza buti taji ni lako tu mwaka huu.
Has Mon, 07th Jul 08 - 11:15 am
Keep it up.....
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 13 guests online and 2 members online
Bongo carlz
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com