SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Msako wa Machangu wapamba moto PDF Print E-mail
Friday, 04 July 2008

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikiliwa wasichana 12 kwa tuhuma za kukutwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama changudoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Marck Kalunguyeye amesema kuwa tukio hilo limetokea leo saa alfajiri, katika maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Amesema watuhumiwa hao (ambao hakutaka kuwataja majina yao), watafikishwa mahakamani leo.

Nao, wakazi 9 wa Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi pamoja na pombe haramu ya gongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kanda Maalum Dar es Salaam, Faustine Shilogile amesema kuwa watuhumiwa hao walinaswa jana saa 4 asubuhi, Mnyamani na Buguruni Madenge.

Watuhumiwa hao walinaswa wakiwa na bangi gramu 100 pamoja na pombe haramu ya gongo lita tano. Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Said Abdalah (31), Abdalah Fikiri (30), Hassan Amir (32), Zainab Juma (30), Riziki Omary (26), pamoja na wenzao wanne.

Pia, wakazi wanne wa jijini wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na puri moja ya bangi na gongo lita moja. Watuhumiwa hao walinaswa jana saa 3 asubuhi, Feri ambao nao ni Abdul Hemed (18), Dadi Said (32), Salum Ahmed (25) na Juma Abdalah (25). Watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
Msambaa - ?? Wed, 09th Jul 08 - 12:29 pm
Kuwakamata itasaidia kuondosha ufukara uliowafanya wawe machangu?
Wapeni vijana ajira ili wajua thamani ya miili yao. watoto kwakukosa ajira ndio wanaamua kuuza miili yao.
GAUCHO Thu, 10th Jul 08 - 06:33 am
kuwakamata sio suluhisho na hiyo biashara sasa imeenea karibia ulimwengu mzima,mana bongo inashamiri kutokana na kuwa kuna wateja kibao wanaowafuata hao madada poa na hii inatokana na mazingira ye2 bongo unakuta wanaume wengi kutongoza ni kazi kwao,pili wanawake nao kama hauna kitu au una kazi ya maana kupata alietulia ni tabu,vilevile matatizo ktk ndoa nyingi nazo zinafanya wengi wanaume kufuata madada poa na hata pengine wanawake walioachika na hawana la kufanya kujitumbukiza ktk hii biashara,kwahiyo kuwakamata machangudoa pekee sio suluhisho kuna vitu vingi vinachangia hiyo biashara ishamiri navyo viangaliwe pia,mana nchi zilizoendelea biashara hiyo ipo lakini watu hawajachizika sana kihivyo na madada poa wengi wana mademu zao labda watalii,waliotengana na wake zao wengi wao ndio wateja wazuri wa machangudoa ila bongo sasa inatisha mana sio tamaduni ye2 na imekua ka fasheni na wateja wengi vijana wazee na wengine wana ndoa zao wanafanya kimbilio huko kwa madada poa,na ndio inafanya nao madada poa waone biashara ya kuuza mwili inalipa kwao pasipo kujali afya zao .
Msambaa Thu, 10th Jul 08 - 10:38 am
Gaucho unachekesha, eti wanaume wengi kutongoza ni kazi LOL.
Na wanaumepia wenye heshima zao hawaendi namachangudoa.
Jambokubwa linalochangia ni umasikini, hatakama mwanamke sio changu lakini kwa wakati huu ukilala naye lazima umpe chochote wakati huku Ulaya unalala na mwanamke lakini humpi hata senti moja.

Gaucho machangudoa walikuwepo toka karne ila siku hizi wako waziwazi, ukisema sio utamaduni wetu nisawa lakini kuna makabila mengine sitaki kuyataja, hao ndio walikua wanasifika zamani hasa kwenye miji mikuu kabla kuja jina la machangudoa.
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20238 registered
female 5034 female
male 15122 male
month 235 new this month
New: uncle g
Who's Online Now
We have 38 guests online and 5 members online
PKJ MaryAnn FESKAM aliciak2 babas
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com