SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register





Kifo cha Raisi wa Zambia Utata PDF Print E-mail
Friday, 04 July 2008

Mwanawasa_1.jpg

 

Rais wa Zambia Mheshimiwa levy Mwanawasa ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amedaiwa kufariki dunia jana asubuhi akiwa hospitalini jijini hapa.

Mauti hayo inadaiwa yalimkuta Rais Mwanawasa baada ya kuugua kiharusi tangu mwanzoni mwa wiki hii, hasa baada ya kulalamikia maumivu makali kifuani.

Hayo yalielezwa jana na Msemaji wa Ubalozi wa Zambia nchini hapa, ingawa hakukuwa na tamko lolote kutoka kwa maofisa wa Zambia.

Aidha Rais Mwanawasa (59), alikimbizwa hospitalini Jumapili wiki iliyopita, alipokuwa mjini Sharm-el-Sheikh, Misri, baada ya kuugua kiharusi ghafla kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 11 wa Umoja wa Afrika (AU).

Ilielezwa kuwa alihamishiwa jijini hapa kwa matibabu zaidi na uchunguzi na baada ya hapo alifariki dunia. Rais Mwanawasa kabla ya kifo chake alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo imekuwa msuluhishi mkuu katika mgogoro wa kisiasa unaoikumba Zimbabwe.

Kiongozi huyo aliwahi kuugua kiharusi mwaka juzi, lakini kabla ya kuchaguliwa tena mwaka huo, alithibitisha kuwa afya yake ni salama na hana tatizo lolote.

Alitarajiwa kutoa msimamo wake mkali dhidi ya uchaguzi wa Zimbabwe katika mkutano wa AU, ambako alipangiwa kukaa jirani na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, kwa mujibu wa alfabeti za majina.

Kiongozi huyo alisikitishwa na kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Bw. Morgan Tsvangirai, kulazimika kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais, kutokana na vitisho dhidi ya wafuasi wake.

Hata hivyo, habari kutoka Lusaka, Zambia, zilimkariri Makamu wa Rais akikanusha habari za kifo cha Rais Mwanawasa akisema bado anaendelea na matibabu hospitalini Paris.

"Rais jana alilala vizuri katika hospitali ya kijeshi ya Percy Ufaransa. Habari zilizotangazwa ... si za kweli," alisema Makamu wa Rais, Bw. Rupiah Banda, katika taarifa yake.

Mapema jana, kituo cha redio cha Talk Radio 702 cha Afrika Kusini, kilitangaza kuwa Rais Mwanawasa amefariki dunia kikiukariri Ubalozi wa Zambia nchini humo.

Akiungwa mkono na Waziri wa Habari wa Zambia, Bw. Mike Mulongoti, Bw. Banda alisema Rais Mwanawasa alikuwa akitibiwa shinikizo la damu.

"Madaktari wanaomhudumia wameridhishwa na maendeleo yake na hali yake inaendelea vizuri. "Ameendelea kupata matibabu ya shinikizo la damu katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU) na hakuna mabadiliko yoyote," alisema Bw. Banda.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
ferrari - Mnatujaribu au? Fri, 04th Jul 08 - 01:10 pm
Kama ni kweli Mh.Rais wa Zambia amefariki basi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi! Na kama uyo Makamu wa Rais anaturusha basi ******ndu wake!
Big tymers - Levy makes progress Fri, 04th Jul 08 - 08:26 pm
DOCTORS attending to President Mwanawasa in France are happy with the progress that he has so far made after his admission to Percy Military Hospital in Paris on Tuesday.
Vice-President Rupiah Banda said yesterday in a statement in Lusaka that Dr Mwanawasa was still alive and had continued to receive treatment for hypertension in the intensive care unit (ICU).

Mr Banda refuted reports by the international media that President Mwanawasa had died.

SOMA ZAMBIA DAILY MAIL
http://www.daily-mail.co.zm/media/news/viewnews.cgi?category=2&id=1215152031
GAUCHO Sat, 05th Jul 08 - 03:29 am
hii ni kama Sharon wa Israel na baba wa taifa ni nguvu za mashine tu sasa mana sio yeye.yote tunamwachia mwenyezi Mungu ana yeye ndie mtoaji na mtwaaji ameni!
TalibKweli - Luca pls update!!! Sun, 06th Jul 08 - 09:46 am
Vipi Luca hii imekaaje? huu mtandao umezidi kuwa maarufu,please update your news na uwe makini na source zako... huyu Dingi bado anatweta, watch out Bro watakushtaki Wazambia Oooh!
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 19348 registered
female 4821 female
male 14445 male
month 666 new this month
New: KITOJO
Who's Online Now
We have 36 guests online and 14 members online
Marc hustlla my rachel halfa k nyaksy darkchild.inc Rashid10 sifa Elmi faddymbongo Thabit tudes underdoggy kitoeo
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com