SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register





Makamuzi bado yanaendelea UK-Jide PDF Print E-mail
Thursday, 03 July 2008

jaydee_jap_l.jpg

 

Judith Wambura a.k.a Binti Machozi a.k.a Lady JayDee kama unahofia kuchapia waweza kumuita Jide, bado anaendelea na ziara yake nchini uingereza ambapo anatarajia kupiga show nyingine mbili kabla hajarejea, kesho atakuwa Club Afrique jijini London wakati Juma Mosi atakamua ndani ya Birmingham.

Jide ambaye kwa sasa yupo katika mji wa Manchester alizungumza na bongo5.com kwa njia ya mtandao na kusema kuwa anatarajia kutua bongo mara tu baada ya kumaliza show hizo mbili ambazo zimeandaliwa na watanzania waishio huko.

“Huwa naamini jitihada pekee ndio zinaweza kumfanya msanii kufikia hapa ambapo mimi nimefikia, so napenda mashabiki wasidhani nimewasahau namalizana na hivi vimeo then Ijumaa Machozi Band kama kawa katika viwanja vya zamani kwani nitatua bongo tarehe 10” alisema Jide.

Hii inaonesha wazi kuwa oneho ambalo ndio lilikuwa sababu ya Jide kwenda UK limezaa maonesho mengine mawili, “Yeah nilikuja tu kwa ajili ya Mandela lakini nimeweza kukutana na show nyingine mbili, sasa hii ni kazi yangu hivo ningependa ifahamike kuwa makamuzi bado yanaendelea pande hizi”-Lady Jay Dee.

Mwanadada huyu anatamba sana na ngoma zake ambazo zimekuwa zikiwashika mashabiki wa muziki wa Tanzania ulimwanguni, alijipatia bahati ya kwenda kufanya onesho katika sherehe ya kuzaliwa Raisi wa zamani wa Afrika kusini mheshimiwa Nelson Mandela iliyofanyika nchini Uingereza wiki iliyopita.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
davidsamuel - jay dee Fri, 04th Jul 08 - 12:00 am
:cheer: namfagilia sana lady jay dee
ssauti pinavutia mashabiki wengi
iaTanzania analetea Tanan jina nzuri kutrumia muziki
brother I Fri, 04th Jul 08 - 06:04 am
ndio umemfagilia jide,lakini kama ujui kiswahili andika tu lugha ya kikwenu,kwani b5 haibagui watu wa nchumbiji au wa kutoka ko**te duniani.ni ushauri tu
Has - njomba Mon, 07th Jul 08 - 11:22 am
Wacheni pujo hijo jama wacheni ukalopi huyu mwanamwali anajua nziki eh.. njini kuyoha hapa we
brother I Wed, 09th Jul 08 - 05:34 am
ndio Has,fagilia kinyumbani...nimecheka,yaani imetulia kinoma
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 19348 registered
female 4821 female
male 14445 male
month 666 new this month
New: KITOJO
Who's Online Now
We have 38 guests online and 11 members online
Marc my rachel halfa k nyaksy BUDDY Rashid10 sifa Elmi faddymbongo Thabit tudes
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com