SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

AU sasa kumjadili Mugabe Misri PDF Print E-mail
Monday, 30 June 2008
MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, akitua nchini Misri
na Mwandishi Wa Tanzania Daima


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, ameondoka nchini jana kwenda Misri, kuhudhuria kikao cha 11 cha wakuu wa nchi za Afrika, kitakachofanyika mjini Sharm El Sheikh, ambako, pamoja na mambo mengine, kitazungumzia hali ya kisiasa nchini Zimbabwe.

 

Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichotanguliwa na kikao cha siku mbili cha 16 cha kawaida cha Baraza la Utendaji la AU, kilichoanza June 27, mwaka huu, chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Tanzania, Bernard Membe.

 

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imeeleza kwamba mada kuu katika kikao cha wakuu wa AU ni maji na usafi wake, chini ya mada ya jumla ya juhudi za Afrika kutekeleza maazimio ya milenia.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kikao kitapokea na kujadili ripoti ya Kamati ya Wakuu 12 wa AU kuhusu kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Afrika, ambapo mjadala kuhusu suala hilo unaendelea tangu Libya ilipotoa pendekezo la kuanzishwa kwa serikali hiyo mwaka 2005.

 

“Ripoti itawasilishwa na Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, iliyokutana katika kikao chake, Arusha, Mei 22 na 23, mwaka huu, “Mbali na Tanzania, nchi nyingine yenye wajumbe katika kamati ya wakuu 12 ni Ghana, Senegal, Libya, Misri, Botswana, Afrika Kusini, Ethiopia, Uganda, Gabon na Cameroun ambazo zote zilihudhulia mkutanao wa Arusha,” ilieleza taarifa.

 

Ilifanunua kuwa kikao cha Sharm El Sheikh kitajadili na kufikia uamuzi kuhusu pendekezo la kuunganishwa kwa mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu na Waafrika pamoja na mahakama ya AU.

 

Kikao hicho pia kitateua majaji wanne wa mahakama hiyo kati ya majaji saba wanaowania nafasi hiyo.

 

Pamoja na hayo, kikao kitapokea na kujadili ripoti ya shughuli za Baraza la Amani na Usalama la AU. Mjadala huo utagusia hali ilivyo katika nchi za Comoro, Burundi, Ivory Coast, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Somalia, Darfur na Zimbabwe.


Source: Tanzania Daima
Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
Ancojak - Kila la kheri Mon, 30th Jun 08 - 11:59 am
Mungu saidia huo mjadala ulete mabadiliko yenye mafanikio na amani kwa africa. na Mugabe mbona sijaona mwakilishi wake? ndio kusema yeye hahudhurii?????????????????, Ebo!!!!!!!!!!! :woohoo:
Kenn - Shime JK Mon, 30th Jun 08 - 07:41 pm
:dry: Unayo kazi kubwa mbele yako Mh. Jakaya mrisho Kikwete sio tu barani africa bali pia hapa bongo (Tz). Hali ya Zimbabwe bado ni tete lakni pia wabongo bado macho yao ya yamatamanio ya maisha bora bado yameelekezwa kwako. Kupanga ni kuchagua, weka vipaumbele vyako kiumakini ili utimize ahadi zako. Muombe Mungu wa Daniel atakusaidia. nasi wabongo tunakuombea Mungu akupe hekima na maisha marefu.
ferrari - Maskini Mugabe! Wed, 02nd Jul 08 - 10:17 am
We Mugabe unajua kabisa una makosa kwanni ucombe radhi kwa Mungu wako,Wananchi wako na Wakoloni kabla ujafa? Unasumbua viongozi wetu bila malipo yyte!
Big tymers - kwanza nyumbani Wed, 02nd Jul 08 - 09:17 pm
kabla ya kuangalia suala la zimbabwe, tuangalie suala la kwetu nchini,richmond,loliondo na sehemu zingine.....je mikataba na walaghai imekwendaje?
vile vile je wale wanyama waliokuwa wanapelekwa SAUDIA ulikuwa mkataba wa nani ..and then tuingilie kimataifa sio mbele mbele tuu kwenye mada za watu, zetu mbilinga
mugabe anadai ardhi yake, waacheni watapata ufumbuzi na mpinzani wake, yetu bado hatujamaliza tunakimbilia ya watu
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 17 guests online

Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com