SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register





Nyumba za wageni ziweke kamera kunasa matukio-Kova PDF Print E-mail
Monday, 30 June 2008
Na Anneth Kagenda

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova, amezitaka hoteli zote na nyumba za kulala wageni kuweka kamera za kunasa matukio.

Amesema kamera hizo zitakazokuwa zinaonyesha watu wanaoingia na kutoka hotelini hapo zitakabiliana na ujambazi ulioshamiri wa kutumia silaha.

Kadhalika, amewataka wahudumu wa nyumba hizo kuvaa sare na vitambulisho ili waweze kutambulika kwa urahisi kuwa yupi ni muhudumu na yupi ni ngeni.

Kamanda Kova alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni na madereva taksi, uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kuimarisha usalama katika maeneo yao.

Vile vile aliwataka wamiliki wa hoteli hizo kuweka vitabu kwa ajili ya kuandika majina ya watu wanaoingia.

Alisema wako watu ambao wanakawaida ya kutoandika majina yao kwa vile wanafahamiana na wamiliki hao na kwamba wanashutumiwa kuwa ni miongoni wa majambazi wanaofugwa ndani ya nyumba hizo.

``Agizo hili nalitoa kwa vile wako wanaofika katika hoteli zenu na kujifanya wateja kumbe wamefika kwa ajili ya kufanya uhalifu na kuiba mali za watu na ukiangalia jina lake kwenye kitabu hulioni hivyo nikisema kuwa wamiliki wanakuwa wanawajua nakuwa sijakosea,`` alisema Kamanda.

Aidha, alisema ikiwa wamiliki hao watafanya hivyo basi ujambazi wa kujificha kwenye nyumba hizo unaweza kupungua.

``Nyumba hizo huwa zinatuhumiwa mara kwa mara kwa kuwalea majambazi na mizigo ya wageni inaibiwa mara kwa mara hivyo iwapo tutashirikiana na jeshi la polisi nina imani uhalifu utapungua kwa kiasi kikubwa,`` alisema Kamanda Kova.

Kwa upande wa madereva taksi, Kamanda alisema kuanzia leo ndio mwisho wa magari yasiyosajiliwa kufanya biashara ya teksi jijini Dar es Salaam, na kwamba baada ya leo gari litakaloonekana likikaidi amri hiyo likamatwe mara moja.

Aliongeza kuwa ikiwa mtu anataka kufanya biashara hiyo basi asajili gari kwa utaratibu uliowekwa na si kutumia usafiri huo bila vibali kwa sababu magari hayo yanashutumiwa kwa kuwabeba majambazi na wauzaji wa madawa ya kulevya.

Source: Nipashe

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
mtemi - wageni kunaswa kwenye video Thu, 03rd Jul 08 - 08:12 am
sasa mkisha wanasa hao wageni na vitendo vya ndani ya vyumba vya hoteli mtatuuzi hizo picha za vitukoo au mtampa huyo mheshimiwa aburudike nazoooo
Nisipitwe - Mh!!!!! Thu, 03rd Jul 08 - 12:06 pm
Aaaaa wapi hiyo si solution ya kuzuia mijizi.
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 19501 registered
female 4850 female
male 14569 male
month 98 new this month
New: carter
Who's Online Now
We have 19 guests online and 2 members online
zeed automaticciera@aol.com
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com