SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Tamasha La 11 La Nchi za Jahazi PDF Print E-mail
Saturday, 28 June 2008

Kwa mara nyengine tena Tamasha la kumi na moja (11) la nchi za Jahazi litafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 11 hadi 20 Julai ya mwaka huu wa 2008.

 

Tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe unaofahamika kama ‘Culture Crossroads’ ikiwa na maana ya mikinzano ya utamaduni. Hii ikiwa ni kukumbusha mahala ambapo jamii ya nchi za Jahazi inapotokea na jinsi ambavyo ilivyochanganya utamaduni kutoka karibu ya kila pembe ya dunia

 

Mgeni maalum katika tamasha la mwaka huu anatarajiwa kuwa ni Ramsey Noah, msanii maarufu wa maigizo kutoka nchi ya Nigeria. Ramsey Noah aliyezaliwa mwaka 1973 ni muigizaji maarufu ulimwenguni anayefahamika sehemu kadha ikiwemo hapa Tanzania kutoka na uahiri wake wa kuigiza, miongoni na filamu zake zilizomjengea sifa ni pamoja na To Love an Angel (2007), Consequences (2006), Dancing Heart (2006), Different World (2006) na Under the Sky (2006).

 

ziff.jpg

 

Katika tamasha la mwaka huu zaidi ya filamu 50 zinatarajiwa kuonyeshwa. Miongoni mwa filamu hizo ni pamoja na Behind this Convent (2008) iliyotengezwa Rwanda, Hero - wings are not necessary to fly (Spain) ya mwaka 2007, Pukwa (2008) nchini Kenya, The Great Silence (2008) USA, One Day (2006) Norway, Jando (2006) Tanzania, An Islamic Conscience the Aga Khan and the Ismailis (2008) UK na The Princess from Zanzibar (2007) German. Mbali ya filamu katika tamasha la mwaka huu pia kutakuwepo na vikundi zaidi ya 30 kutoka Tanzania, Msumbiji, Malawi, Comoro, Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe na kutoka bara la Asia. 

 

Katika tamasha la mwaka huu vikundi vyote vya muziki vitakavyoshiriki vitawezeshwa na ZIFF kuweza kutumia vifaa vya muziki moja kwa moja bila kutumia play back wanapokuwepo jukwaani.

 

Kama kawaida tamasha la mwaka huu pia kutakuwepo na jukwaa la vijijini, wanawake na watoto ambapo filamu, warsha na maonyesho kadhaa yatafanyika katika majukwaa hayo.

 

Tamsha a nchi ya Jahazi ni tamasha kubwa la utamaduni na filamu katika Afrika Mashariki na kati linalofanyika kila mwaka mara moja tokea mwaka 1998.


Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu www.ziff.or.tz or wasiliana na:

ZIFF Media and PRS Office
Tel: +255 (0) 777 411499 Fax: +255 (0) 777 419955
Website: www.ziff.or.tz E-mail: This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 13 guests online and 2 members online
Bongo carlz
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com