| Tabata Dampo Kimenuka tena |
|
|
|
| Friday, 27 June 2008 | |
|
Watu wanaodhaniwa kuwa wakazi waliokuwa wakiishi katika eneo la Tabata Dampo jijini Dar es Salaam na watumishi wa kampuni inayodaiwa kuwa ni ya mmiliki wa eneo hilo, Alied Cargo wamefikishana polisi baada ya wamiliki hao kudaiwa kuvamia eneo hilo ikitaka kuweka uzio kwa ajili ya ulinzi. Hatua ya kufikishana polisi imetokea kufuatia vurugu zilizotokea baina ya wakazi hao na wafanyakazi hao wa Alied Cargo baada ya watu hao kuwakuta wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiweka uzio katika eneo hilo. Kwa upande wake meneja wa Alied Cargo amedai kuwa baada ya kuona wakazi hao wamehama katika eneo hilo walipeleka madai ya kumiliki eneo hilo kwa manispaa ya Ilala kwani wana nyaraka zinazowathibitisha kuwa wao ndio wamiliki halali wa eneo hilo.
|
| < Prev | Next > |
|---|







