| Werrason Atua Jijini…Show Uhakika |
|
|
|
| Thursday, 26 June 2008 | |
|
Hapo awali ilipotangazwa ujio wa msanii huyu nchini alisubiriwa kwa hamu na hakutokea lakini kwa uhakika zaidi mkali huyu ameshawasili nchini na anatarajiwa kupiga show ya kufa mtu hapo kesho ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza. Werrasone akiwa ameambatana na kikosi chake amewsili majira ya saa tano usiku leo na kupokelewa na Mkurugenzi wa Clouds Entertanment Joseph Kusaga, onesho hilo limedhaminiwa na kampuni ya TCC chini ya usimamizi wa sigara yake ya Embasy. Aidha imedaiwa kuwa Baada ya onesho hilo la kwanza hapa Dar Werrason ataelekea mkoani Arusha ambako huko nako atapiaga show moja katika ukumbi wa Naura. Aidha waandaaji hao wameweka dhahiri kuwa maandalizi ya onesho yamekamilika na kiingilio kitakuwa ni sh 20,000 halikadhalika kutakuwa na msosi wa kufa mtu kwa watakahudhuria show hiyo. Safari hii haina longo longo wala nini…Werrason ypo nchini na atafanya makamuzi hapo kesho. Werrason amekuwa akitamba sana na vibao kadhaa wa kadha ambavyo vimekuwa ni gumzo ile mbaya jijini na hta ulimwenguni kwa ujumla, hivyo wapenzi wa muziki nchini Tanzania watarajie burudani ya ukweli.
Mkurugenzi wa Clouds Entertainment akimpokea Werrason Airport.
|
| < Prev | Next > |
|---|







