SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Mb Dog anakomesha Kenya na Uganda PDF Print E-mail
Thursday, 26 June 2008

mb_dogg_m.jpg

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye hivi karibuni amezungumza na Bongo5 na kudai katika hatua za mwisho kuweka albam yake sokoni, ambapo mpaka sasa amekuwa akipokea idadi kubwa ya simu kutoka nchi za Kenya na Uganda zikimtaka akapige show huko.

“namshukuru sana mungu kwa kunijaalia kipaji sema ninachozingatia ni kujipanga zaidi kwani naamini show zipo nyingi zinakuja hasa mara nitakapomliza mazungumzo na wadosi kuhusiana na kuiweka ablam yangu kwenye soko hivyo sina harka kabisa” alisema Mb Dog.

Msanii huyu amechomoka na ngoma yake mpya ambayo imeonekana kuwa ni gumzo ile mbaya jijini akiwa ameifanyia katika studio za 41 chini ya usimamizi wake prodyuza Ambrose, inayokwenda kwa jina la ‘naona raha’ kama kawaida yake jamaa huwa hafanyi ajizi linapokuja suala la kuimba nyimbo za mapenzi.

Albam ya msanii huyu inakwenda kwa jina la ‘Akili yangu’ ambayo ameifanya katika studio tofauti ikiwemo 41 Records, Bongo Records, Up Town Records “unajua huwa nina kawaida ya kukaa kimya muda mrefu lakini napotoka huwa nahakikisha sibahatishi hiyo wale ambao wamekuwa wakinimiss jukwaani wasubiri kidogo tu show za tofauti na za ukweli zinakuja”-Mb Dog.

Mb Dog ambaye kwa sasa amekuwa gumzo nchini Kenya na Uganda hasa baada kuiweka singo yake mpya hewani hali ambayo inaashiria mwanzo mzuri wa ujio wa albam yake mpya ambayo anatarajia kutoka nayo.

“Licha ya Kenya na Uganda pia hapa bongo mapromota wamekuwa na moto ajabu kila kukicha napokea simu nyingi zikinitaka nikapige show sehemu tofauti lakini naamini time yangu bado soon ziara zitaanza watu wangu msikonde wala nini” alimaliza.

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20238 registered
female 5034 female
male 15122 male
month 235 new this month
New: uncle g
Who's Online Now
We have 38 guests online and 5 members online
PKJ MaryAnn FESKAM aliciak2 babas
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com