| Ghorofa lililoanguka Dar…uchunguzi bado |
|
|
|
| Wednesday, 25 June 2008 | |
|
Zikiwa zimepita siku nne tangu kuanguka kwa jingo lenye urefu wa ghorofa kumi jijini lililopo katika mtaa wa kisutu na Mtendeni kisanga kingine chazuka baada ya watanzania kutaka kujua sababu za kufichwa kwa ripoti ya kamati ya uchunguzi wa majengo jijini Dar Es Salaam. Jengo hilo ambalo lilianguka mbele ya raia na waandishi wa Habari, viongozi wa Serikali, na aliyfahamka kama muhandisi wa jendo hilo, katika hali ya kusikitisha baadhi ya raia walikuwa ndani ya kifusi huku wakiwapia simu ndugu, jamaa na marafiki akiaga na kuelezea hali ambayo ilikuwa imewafika kwa wakati huo. Jengo hilo ni mali ya Kampuni ya Mcsoms Investment Ltd, ambapo tangu saa tatu asubuhi ya siku hiyo lilianza kuonesha dalili mbaya pale baadhi ya viunga vyake vilivyoanza kumong'onyoka na kudondoka chini huku upande mmoja ukiwa unatitia aridhini taratibu huku sehemu ya aridhi ikionesha mipasuko. Baada ya jengo hilo kuanguka ilitolewa amri na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Abbas Kandoro na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova, ya kuwataka watu, kampuni za ulinzi,mashirika yenye vifaa vya uokoaji kufika eneo la tukio kutoa msaada. Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Jijini, Bw. Fikiri Salla, amesema mwili wa marehemu Shamte ambao ilionekana kuwa mgumu kupatikana hatime ulifukuliwa katikati ya kifusi juzi asubuhi, mishale ya saa 11:00 ambapo mpaka sasa taratibu za mazishi zimeshakamilika. Akasema mtu huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ghorofa la jirani lililopo kwenye Mtaa wa Kisutu, ambalo liliaathirika baada ya kuporomokewa na jengo la ghorofa kumi lililoanguka asubuhi ya juzi na kuwajeruhi watu kadhaa. “Leo asubuhi tumefanikiwa kumpata mtu wa nne akiwa amefukiwa na kifusi... lakini kwa bahati mbaya, yeye alikuwa ameshafariki dunia” alisema Bw. Salla. Bw. Salla akasema maiti ya mtu huyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akielezea juu ya zoezi la uokoaji, amesema kwa ujumla, watu wanne ambao waliambiwa kuwa ndio waliokuwa wamenasa ndani ya jengo wameshatolewa wote, akiwemo marehemu Shamte. Akasema wengine watatu walishaokolewa baada ya kukutwa ndani ya masalia ya jengo lililoporomoka wakiwa hai. Hata hivyo baada ya waandishi wa habari kufika katika jengo hilo kabla halijaporomoka, walimuhoji Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Robert Masola kuhusu ubora wa jengo hilo, ambaye aliwajibu kuwa ubora wa jengo hilo ni wa uhakika na haliwezi kudondoka kwa namna yoyote ile. Haukupita muda mrefu mara jengo hilo liliporomoka na Masola alipigiwa simu, na aliporejea aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kile kilichoelezwa na polisi inamhitaji zaidi Mhandisi wa Manispaa ya Wilaya ya Ilala pamoja na mkandarasi wa jengo hilo kwa sababu ndio wahusika wakuu waliokuwa wakisimamia ujenzi wake. Baada ya tukio hilo, baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisimamishwa kazi na wengine kuhojiwa. Pia serikali ilitoa tamko la ukaguzi wa majengo mbalimbali ya ghorofa katika Jiji la Dar es Salaam baada ya baadhi kushukiwa kujengwa kiholela. Pamoja na hayo yote ni raia mmoja ambayo alikuwa akisakwa na baadhi ya raia na pia kikosi cha zimamoto ambacho kiliweza kuwepo katika harakati za kujaribu kuokoa. Katika tukio hilo, watu walioshuhudia walisema kuwa dalili za jengo hilo kutaka kuanguka, zilionekana tangu mapema na watu walipewa taarifa za kutoka ndani ya jingo na eneo hilo kwa ujumla. Mmoja wa walioshuhudia, Bw. Mahafudhi Jumaa (60) alisema dalili za kuanguka jengo hilo zilianza kuonekana tangu kuanza kwa ujenzi. Wakazi wa eneo hilo walifikia hatua ya kupeleka malalamiko kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuhusu ujenzi usiozingatia viwango lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. “Jengo hili tulijua litabomoka kwa jinsi lilivyokuwa likijengwa bila kuzingatia viwango, tumelalamika hawajataka kutusikia, lakini tunadhani ni kwa sababu ya rushwa” alisema. Mhandisi Msaidizi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Robert Massoro aliyefika katika eneo la tukio alijikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Kati. Mhandisi huyo alikamatwa na polisi kwenye eneo la tukio wakati akiendelea kuhojiwa na waandishi wa habari ambao walikuwa wakimuuliza hatua alizochukua tangu kuanza kwa ujenzi huo. Bw. Massoro alisema kuna watu waliokuwa wakikagua kila hatua ya ujenzi wa jengo hilo hivyo asibebeshwe lawama kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi ukifanyika ukweli utabainika. Alipobanwa na waandishi wa habari kuwa jengo lilijengwa bila kuzingatia viwango, alijibu kwamba uchunguzi wa kubaini kuwa lilijengwa chini ya kiwango hauwezi kufanywa kwa kuangalia kwa macho. Idadi dhidi ya walokuwepoa katika jengo hilo bado haijawa ya uhakika lakini mpaka sasa ukaguzi unaendelea na iwapo taarifa kamili kuhusiana na wajeruhi na waliofariki itawekwa wazi na kuhakikisha kila penye uzembe pachukukuliwe hatia kali za kicheria.
|
| < Prev | Next > |
|---|







