SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Dos Santos kuongoza mjadala wa Mugabe PDF Print E-mail
Wednesday, 25 June 2008

eduardo_1.jpg

 

Jumla ya Maraisi watano wa nchi za Kusini mwa Afrika, wanatarajia kukutana leo ili kujadili hali ya Zimbabwe chini ya Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola.

Wengine watakaoshiriki mkutano huo, ni Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Zambia, Bw. Levi Mwanawasa.

Marais wengine ni Msuluhishi wa Nchi za SADC katika Zimbabwe, Rais wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki na Mfalme Mswati III wa Swazilandi.

Mkutano huo ni wa Asasi ya Ushirikiano ya SADC ambayo Mwenyekiti wake ni Rais Dos Santos.

Taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilisema Rais Kikwete aliondoka jana mchana kwenda Mbabane, Swazilandi kwa ajili ya mkutano huo.

Mkutano huo kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni wa siku moja na utajadili jinsi SADC na asasi hiyo vinavyoweza kuisaidia Zimbabwe kuondokana na hali yake ya sasa ya machafuko.

Zimbabwe inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa marudio wa urais ambao umepangwa kufanyika keshokutwa, huku mgombea wa Movement for Democratic Change (MDC), Bw. Morgan Tsvangirai akiwa ametangaza kujitoa.

Bw. Tsvangirai ambaye katika uchaguzi wa awali alipata ushindi mwembamba hivyo kutokidhi kuongoza nchi, amekuwa akidai kuwa uchaguzi huo wa marudio hauwezi kuwa huru na wa haki kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
msemakweli - Babu amka!! Wed, 25th Jun 08 - 06:00 am
ushauri wa maana kwa kiongozi mkongwe kama mugabe ni kung'atuka tu na si kungaganiza watu nchi imemshinda. kama hasikii UN itamnyoosha!!!!!!
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 16 guests online

Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com