SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Kuhama Dodoma Mjadala ufanyike PDF Print E-mail
Tuesday, 24 June 2008

pinda_m.jpg

 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amedai kuwa serikali itaendelea kuendesha mjadala wa kitaifa utakaowashirikisha wadau mbalimbali dhudu ya suala la kuhamishia Makao Makuu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Aliyasema hayo katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi yake aliyoisoma bungeni jana, baada ya mjadala huo kwamba serikali itaandaa mapendekezo ya kutunga sheria mpya ya kutambua rasmi Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali.

Waziri Pinda pia alizungumzia maslahi ya Madiwani na kueleza kuwa katika mwaka ujao wa fedha Sh bilioni 4.8 zimetengwa kwa ajili ya posho za madiwani.

Aidha alidai kuwa sheria ya Bima ya Afya ambayo itawawezesha madiwani kupata matibabu kupitia mfuko huo, halikadhalika itaandaa marekebisho ya sheria ya fedha yatakayofanyika ili madiwani wafaidike na msamaha wa kodi kwa vyombo vya usafiri.

Alisema Jiji la Dar es Salaam kwa sasa linakabiliwa na miundombinu ya barabara isiyokidhi mahitaji yanayopanuka kila siku na miundombinu ya maji safi na taka na ukuaji wa jiji usioenda sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Hali hii inalifanya jiji lisionekane kama kioo cha nchi yetu, Kuna haja ya kuwa makini sana katika hili.” – Pinda.

Halikadhalika Waziri Mkuu pia alizungumzia muundo wa Jiji la Dar es Salaam ambalo lina manispaa tatu zinazojitegemea na kueleza kuwa uzoefu wa miaka minane wa utekelezaji wa mpango huo umeonyesha kuwa muundo huo una matatizo ya uendeshaji na hivyo kutokidhi matarajio yaliyokusudiwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kuhusiana na ujenzi wa miundombinu utaanza rasmi katika mwaka ujao wa fedha na utachukua miezi 24. Pia alizungumzia uchaguzi wa vitongoji ambao utafanyika Oktoba mwakani na kueleza kuwa Sh bilioni 4 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo ikiwamo kuhakiki mipaka ya vitongoji, vijiji na mitaa, kufanya mapitio ya kanuni za uchaguzi na kufanya mikutano ya ushauriano na vyama vya siasa.

Bila kusahau kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa, Pinda alisema katika mwaka ujao wa fedha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali utafanyika na mkazo zaidi utawekwa kwa tuhuma za mikataba mikubwa ambayo inaiingizia serikali hasara.

Akizungumzia sekta ya madini, Pinda alisema migodi mingi ya madini hasa ya wachimbaji wadogo haiko salama hivyo akatoa mwito suala hilo kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuhakikisha kwamba wamiliki wa migodi hiyo wanafuta kanuni zilizopo za usalama migodini kuepuka maafa kama yaliyotokea Mererani.

Kuhusu chakula, alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha zimetengwa Sh bilioni 26.3 kwa ajili ya kununua tani 100,000 za mahindi na tani 5000 za mtama utakaofanywa na kitengo cha hifadhi ya chakula.

Pia amekiagiza kitengo hicho kununua nafaka kutoka kwa wakulima kwa wakati kuzuia uwezekano wa wakulima kuuza chakula kwa walanguzi na nje ya nchi na baadaye kukinunua kwa bei kuwa ya juu.

Waziri Mkuu pia alisema kituo cha uwekezaji katika mwaka unaomalizika Julai kimesajili miradi 902 yenye thamani ya Sh bilioni 8.1 ambayo imetoa ajira kwa Watanzania 127,588.

Alisema kati ya miradi hiyo miradi 483 ni ya Watanzania na 196 ni ya wageni huku miradi 223 ni ya ubia. Kwa upande wa ofisi za wabunge, Pinda alisema ofisi 40 zitakamilika kujengwa katika mwaka ujao wa fedha katika awamu ya kwanza na ofisi nyingine 10 zitaanza kujengwa.

Sh bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kumalizia ofisi za awamu ya kwanza na kuanza ujenzi wa ofisi zilizoko katika awamu ya pili.

 

 

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
bigirwa Wed, 25th Jun 08 - 02:49 am
Ogera pinda kwa kuifikria dodoma maana hii itapunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali. kwani kwa sasa watu wanafanya kazi nusu nusu kwa kuwa na ofisi mbili nyingine dodoma na nyingine Dar kwa hiyo kuhamia dodoma kutatoa nafasi yakujurikana ni wapi serikali ipo.
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 14 guests online

Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com