SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Dr Slaa amtolea uvivu Mkulo PDF Print E-mail
Tuesday, 24 June 2008

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni Dk. Wilbroad Slaa, hivi karibuni aliwasilisha bungeni kile alichosema ni ushahidi kuthibitisha kuwa fedha zilichotwa kutoka akaunti ya madeni ya nje iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilikuwa za serikali na si za wafanyabiashara kama ilivyosemwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo wiki iliyopita.

Dk. Slaa ambaye ni mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisema utafiti ambao kambi ya upinzani imefanya umegundua fedha hizo kimsingi zilitokana na mpango uliojulikana kama “Debt Buy Back Program.”

Alisema EPA imefanyiwa kazi na timu ya Lazard na baadaye ukaguzi wa PricewaterhouseCoopers (France) Novemba 25, 2004. Alisema hata hivyo ukaguzi uliofanywa na Deloitte and Touche 2006 na baadaye kuthibitishwa na Ernst and Young, 2007 ulithibitisha kuwa Kampuni 22 zilifanya biashara na kampuni zinazodhaniwa kuwa “hewa”.

Alisema hata hivyo wafanyabiashara hao, wala wadai wao ambao wako nchi za nje hawakuweka fedha zozote BoT kwa lengo kutimiza masharti ya mpango Debt Buy Back Program kama alivyoeleza Waziri Mkulo.

“Kwa msingi huo fedha zilizoibwa ni za Serikali ya Tanzania,” alisema Dk. Slaa ambaye alidai ana ushahidi wa ripoti mbalimbali zilizofanywa na makampuni ya ukaguzi wa hesabu kwa nyakati tofauti.

Alisema hata baadhi ya kampuni zilizodhaniwa kufanya biashara na kampuni ya Kagoda inayoaminika ilitumika kuchota kiasi kikubwa cha fedha au haziko na nyingine zimekwisha kubadilisha majina yao.

Alisema kampuni hizo ziko Marekani, Japan, Ujerumani, Italia, Ufaransa na nyingine hata anuani zake hazikujulikana. Katika hotuba yake pia alionyesha ushahidi namna kifungu cha 3.25 cha Ukaguzi huo ulishauri kuwa kwa malipo ya zaidi ya Sh bilioni 42.6 uchunguzi wa kina unahitaji kufanyika.

“Taarifa hii haikutolewa wazi kwa Bunge wala kwa Watanzania ambao ndiyo wenye mali hiyo na Serikali ni mdhamini kwa niaba yao tu”

“Katika hali hii inayoonyesha wazi kuwa kulikuwa na kughushi, wakati Waziri Mkulo alipokuwa akijibu alitetea kuwa fedha za EPA si za Serikali…kama siyo za Serikali kwa nini waghushi?” alihoji.

Mbunge huyo alisema fedha hizo zililipwa kupitia benki ya kizalendo ya CRDB. Alisema hiyo ni benki ambayo ilipaswa kuonyesha uzalendo kama zilivyofanya benki za kigeni kama vile Kenya Commercial Bank na Barclays Bank ambazo zilikataa kulipa fedha hizo baada ya kuona kuwa zina harufu ya ufisadi.

“Benki yetu wenyewe ya CRDB haionekani ikichukua hatua zozote zile hata malipo hayo yalipofanyika kwa mkupuo kwa siku moja kwenye matawi tofauti ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam kama vile matawi ya Kijitonyama, Azikiwe, Vijana, Lumumba na Holland,” alisema.

Alisema uongozi wa BoT, Katibu Mkuu Hazina na Waziri wa Fedha walihusika au kuficha au kuzembea na kuficha taarifa za wakaguzi wa Deloitte.

Naibu Kiongozi huyo pia alizungumzia suala la utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Kampuni ya Richmond iliyoingiza nchini majenereta kwa ajili ya umeme wa dharura haujatolewa taarifa. Alisema Kambi ya Upinzani inashangazwa na hali ilivyo, kwani walitarajia Serikali itatoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Aliongeza kuwa maazimio kuhusu watu waliotakiwa kuchukuliwa hatua za nidhamu hayajatekelezwa.

 

 

 

 

 

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
laseko - tanzania goooooooooooo! Tue, 24th Jun 08 - 02:02 am
its amazing to hear such a constructive story onhow the country is dieying slowly!...the issue here is not what we read or listen from the politicians, but what next after all these?......tanzanians!..lets work up and show the way!
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 13 guests online and 1 member online
Bongo
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com