SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Nani Hizbu? CCM au CUF PDF Print E-mail
Wednesday, 14 May 2008

Baada ya kujibu makombora ya chama tawala CCM, sasa Chama Cha Wananchi (CUF) kimebaini wazi kuwa hali imebadilika na kuonekana sasa vyama hivyo vinakitumia chama cha Hizbu ili kuchafuana.

 

Mara tu hatua huyo kudhihiri, imebainika wazi kuendelea kuwepo kwa uhasama kati ya CCM na CUF hususani baada ya kurushiana madongo kisiasa na kupakana matope kwa kuwahusisha viongozi wa ngazi ya juu baina ya vyama hivyo viwili.

 

Ambapo CCM waliokuwa ni wa kwanza kuwatupia dongo CUF kwa kupitia kwa kada wake mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru kwamba chama hicho kina uhusiano wa moja kwa moja na chama hicho cha kisultani cha Hizbu na jana CUF wakajibu mapigo hayo kwamba CCM ndio wana historia ya kuwa na uhusiano na chama hicho cha Hizbu huku wakiwataja viongozi wa ngazi ya juu akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi na mke wa Rais wa Zanzibar Bi Shadya Karume.

 

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ya uanachama wa Hizbu ni pamoja na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yusuf Himid ambaye ni ndugu wa mama Karume ambao wote ni wajukuu wa Sheikh Mohammed Salim Jinja ambaye ni mwanzilishi wa chama hicho cha Hizbu.

 

Achilia mbali viongozi hao, CUF walidai kuna kiongozi mwingine ambaye ni waziri katika Serikali ya Muungano kwamba aliwahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho cha Hizbu ambao ulikuwa ukijulikana kama Youth Own Union (YOU).

 

Kwa majibu hayo mkanganyiko umetanda miongoni mwa jamii kuhusu hasa ni nani kati ya pande zote mbili ambaye anahusika na chama hicho ama vyama hivyo vimeamua kutumia silaha hiyo kuchafuliana majina.

 

Suala hili liliwahi kuibuka ghafla siku chache kabla ya uchaguzi Mkuu uliopita baada ya gazeti moja la kila siku kutoa picha katika kurasa zake inayomuonesha aliyekuwa mgombea urais, Salim Ahmed Salim akiwa na viongozi waliodaiwa kuwa wa Hizbu miaka miaka ya nyuma.

 

Kutokana na picha hiyo Salim alikuja juu akisema kwamba picha hiyo na habari iliyoandikwa zililengwa kumharibia kisiasa ikizingatiwa kwamba zilikuwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika.

 

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kwamba, iwapo vyama hivyo vimeamua kupakana matope kwa njia hiyo basi suala la kufikia muafaka lisahaulike kwani uhasama kati ya vyama hivyo hautaiha bali daima utaendelea.

 

 

Comments
Search
my rachel {space} {title} Thu, 15th May 08 - 10:45 am
mnaipeleka nchi panaya nyie watu ;;;;na nyie ndo mtasababisha vita..kueni na
busara..sisi ndo tutakaoumia nyie mmening,iniza miguu juu..kudadadadeki zenu
wote wana cuf na ccm..
Bigsome {space} {title} Sat, 17th May 08 - 05:14 am
anayekwamisha muafaka ni makamba ni mnafiki namba moja,suala la usalama wa taifa
yeye analiletea mzaha kutukenulia mimeno yake na kuongea kimzaha na kimajungu
kila wakati,kwanza CCM nao ni wachemfu walimuekea nn yule si mtendaji ile nafasi
anatakiwa akae mtendaji na si mtu kama yeye,by the way please nyie watu kama
alivyosema my rachel busara zitawale ktk hili jambo tutakuja kujuta jamani.
Only registered users can write comments!

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 
< Prev   Next >
Total Members
total 21216 registered
female 5270 female
male 15866 male
month 21 new this month
New: Hapines
Who's Online Now
We have 37 guests online and 15 members online
swejacky Amiry said salehe debra kaga haywire preeety Tito Chamillionaire Danielita jeny2 Jozeedaking Tukwa kelly31 Hapines
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com