Lile kundi maaruku katika kituo cha luninga cha EATV la Ze Comedy ambalo limekuwa likiongoza katika kuchana mbavu za watu hapa nchini, hivi sasa halipo tena pamoja na kituo hicho baada ya kumaliza mkataba wao na kugoma kuendelea kufanya kazi na kituo hicho huku wakidai wanataka kuangalia utaratibu mwingine wa kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa kundi hilo bwana Issaya Mwakilasa a.k.a Wakuvanga alidai kuwa “hatuna matatizo kabisa na kituo cha EATV kwani tumefanya nao kazi katika kipindi chote hicho na wamekuwa wakitulipa vizuri sana hivyo hatuna budi kuwashukuru kwa hili, suala la kuacha kufanya kazi na EATV ni uamuzi wetu binafsi wala sio shinikizo la mtu yoyote tumeamua tu kuangalia taratibu nyingine” alisema.
Kundi hilo lilitokea kuwa maarufu sana linalowahusisha wasanii kama vile Joti, Mpoki, Mac Regan, Masanja, Vengu pamoja na Seki, limekuwa ni kitvutiokikubwa sana kwa jamii na kuna tetesi nyingi ambazo zinaendelea kuvuma mtaani zikidai kuwa inasemekana kuwa jamaa wana mpango wa kuangukia pande TBC jambo ambalo halina uhakika, kilichopo ni kutega sikio na kukodoa macho kwenye luninga itajulikana tu machizi wameangukia pande zipi?
Mmmh mmepata promo kubwa kutoka EATV sana karibu pande nyingi za nchi ya Tz wanawafahamu. Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kujijua kwamba mnaweza kufanya kazi nyinyi kama nyinyi, kilichobaki sasa ni kazi, isionekane kuisha kwenu kwa mkataba ndio ikawa kufa kwa kazi nitasikitika ile mbaya. Macho na masikio ya wa bongo sasa wanataka kuona na kusikia je huo ndio mwishoo au kunawengine wanaweza ila walikosa promo kama nyinyi.
hanna
- yap yap
Sun, 11th May 08 - 05:22 pm
sana tuu lemarobu sina la kuongeza yako yanatosha kazeni buti ze comedy
ghettoprince
- duh
Sun, 11th May 08 - 07:06 pm
ila huko mnakoenda .. mjulikane east africa isije ikawa mnaishia dar peke yake..
davidsamuel
- why
Tue, 13th May 08 - 01:15 am
ze commedy mbona hivy billa nyinyi eatv itafraisha sana you guys rock nawafagilia sana mtarudi nimesikit7ika sana kuskia mnaondoka imekuaje tutawamis sans bila nyinyi tutakwepo kwenye uzuni msipote sana mtafanya watu waipore eatv good luck i hope mtarudi
my rachel
- lol
Wed, 14th May 08 - 03:25 am
hapo mmetuangusha jamani wengine hio tbc hata hatuioni...mtakosa mashabiki..kama ilivokua huku eatv,,haya basi mtakavoamua nyinyi..ila ushauri wangu mrudi palepale..eatv,,cz inaangaliwa na east africa nzima,,huko mtakapoamia mtakua dar peke yake..mmenikera;;tulieni sehem moja..
Musie
Wed, 14th May 08 - 04:51 am
Kwanza nawapa big Up 4 ur efforts..maana kumfanya mtu acheke ipo kazi!!! Ila sasa kwanini mnawakatisaha ghafla mashabiki na wapenzi wenu...kwani mlikuwa hamjui kwamba mkataba unakaribia kuishaaa....kwanini msingelifanya taratibu za aidha ku-u-renew au kutafuta namna nyingine ya kuwaburudisha wapenzi wa Zecomdy..kabla ya kumkataba wenu ungali hai??? Au mmekurupuliwaa?? Semeni msituficheee!!!
tatu
- ZE COMEDY
Fri, 23rd May 08 - 02:27 am
[size=large][color=red][b]SHEMEJIIIIIIIIIIIIIIIIII
IIIIIKWANI NIMEBISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA ETI NIMEBISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA YANI SIO SIRI MMETUANGUSHA SANA WAPENZI WA ZECOMEDY WATU TULIKUWA TUNAWAHI KUFIKA HOME SIKU YA ALHAMIS KWA SABABU YENU SASA WHY KWA NINI?????????????????
NAHUKO TBC1 LINI??????????????
AU MNATUZUGALINE NYIE.[/b][/color][/size]