SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register





Balali kusakwa PDF Print E-mail
Friday, 09 May 2008

Na Mashaka Mgeta


 

Serikali imesema itamsaka Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali mahali popote alipo muda utakapowadia.

Kwa mujibu wa ofisi ya Rais, mbali na Dk. Balali, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge, `amewekwa kiporo` ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili kufanyika, na hatimaye kuchukuliwa hatua kulingana na matokeo yatakayopatikana.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bw. Salva Rweyemamu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.

Jana, gazeti hili lilimkariri Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, akisema serikali haijui mahali alipo Dk. Balali, na kwamba timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, inaendelea kushughulikia masuala yote yanayohusiana na Gavana huyo wa zamani wa BoT.

Hata hivyo, katika maelezo yake, Bw. Rweyemamu alisema hatua ya Rais Kikwete kumfukuza kazi Dk. Balali, ilimfanya (Balali) kuwa raia wa kawaida, mwenye uhuru wa kuishi mahali popote anapotaka, alimradi havunji sheria.

Taarifa zilizotolewa kwa mara ya mwisho na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bi. Zakhia Meghji, zilisema Dk. Balali alikuwa katika hospitali moja huko Boston nchini Uingereza, akipata matibabu ya ugonjwa ambao hata hivyo haukujulikana.

``Balali ni raia wa kawaida mwenye mambo binafsi, hivi sasa hatafutwi, lakini ukifika wakati wa kufanya hivyo, serikali itajua yupo wapi na tutampata tu,`` alisema.

Dk. Balali alifukuzwa kazi na Rais Kikwete, baada ya ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na kampuni ya Ernst and Young kubaini vitendo vya ufisadi, vilivyosabaisha upotevu wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Hatua ya kufukuzwa kazi ilitangazwa wakati Dk. Balali, akidaiwa kuwa Marekani kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande mwingine, Bw. Rweyemamu, alisema uamuzi wa kumkamata na kumfungulia mashtaka Bw. Chenge, utafikiwa baada ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kukamilika.

Bw. Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, anatuhumiwa kuhifadhi takribani Dola 1,000,000 za Marekani kwenye benki iliyoko katika visiwa vya Jersey, Uingereza, fedha zinazohisiwa zilipatikana kwa njia ya ufisadi katika ununuzi wa rada, wakati wa serikali ya awamu ya tatu, iliyoongozwa na Bw. Benjamin Mkapa.

``Tukisema tumkamate Chenge sasa hivi, kutakuwa na kelele kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu na hata ninyi waandishi wa habari. Tusubiri uchunguzi ukamilike,`` alisema.

Aidha, alisema Rais Jakaya Kikwete, bado hajafikia uamuzi wa kumtangaza Waziri wa Miundombinu, kuziba nafasi iliyoachwa na Bw. Chenge.

``Suala la kumtangaza Waziri wa Miundombinu litafanywa kwa umma na si kificho, hivyo wananchi wasubiri tu, kwa sababu suala hili haliwezi kufanyika kinyemela,`` alisema.

Pia Bw. Rweyemamu, alisema suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), inastahili kufikiwa kwenye meza ya mazungumzo.

CUF ilitangaza kutoendelea na mazungumzo hayo baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kuazimia kuwa makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto visiwani humo, yanapaswa kupata ridhaa ya wananchi, kupitia kura za maoni.

Msimamo wa CUF ni kwamba suala la kura ya maoni halikuwepo katika ajenda za mazungumzo baina ya vyama hivyo.

 

Source: Nipashe

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
lemarobu - Huo sasa Ufisadi mwingine Fri, 09th May 08 - 12:45 am
Shwain, hakuna lolote mnataka wananchi wamsahau mumuache, mambo yako hadharani kwanini asifanyiwe kazi mapema, acheni mambo ya kulindana mtazidi kuifanya nchi ioze na kunuka. huo uchunguzi nao mnaufanya kifisadi vilevile.Msiwaumize wananchi kwa kutumia madaraka yenu, Shwain
hassans - KUDADADEK Fri, 09th May 08 - 04:02 am
Hakuna kuangaliana machoni kwa suala hilo.Atafutwe haraka iwezekanavyo.Hivi jamani wananchi weneyewe maskini na bado hela zao mnakula hivi hata Mungu hammuogopi?
brother I Fri, 09th May 08 - 05:45 am
mbona wananchi wa kawaida wanasubiri uchunguzi wa kesi zao segerea,lakini hawa wavaa makoti wanalindana tu.wanaafiki wakubwa kwasababu hata wao wenyewe wana dhambi zao,ndio maana kulindana hakutakwisha
Mwafrika - MUNGU SAIDIA TZ Fri, 09th May 08 - 12:41 pm
hawa CCM na siri kali yao wanatufanya wananchi mambumbu jamani,tokea nimesikia habari za Balali kusakwa na kufikishwa mahakamani imeshapita muda mrefu sasa na mtu bado yuko anakula kuku kwa fedha zetu masikini alizozikomba yeye na wenzie wenye mitumbo mikubwa,haya mambo yapo wazi jamani kwamba Balali ni raia tu kama raia wengine hivyo ni wakati sasa umefika bila ya kuoneana aibu kumkamata na akangojelee uchunguzi akiwa Segelea,msitake kutumwagia changa la macho kwa kutuona sisi hatujui sheria za nchi, huu ni ujinga tu wa kufanya unyonjaji kwa wananchi wa kipato cha chini ili mjinufaishe nyinyi mlio madarakani,huyu Balali akamatwe na arudishwe hapa Bongo,mnachunguza nini sasa muda wote huo?ujinga tu,kama hana hatia mbona anakimbia sasa nchi na hadi maswahiba zake wanadai hawajui alipo,mambo gani mnatufanyia nyinyi CCM?ili kuleta angalau imani kwa wananchi ambao tayari wameshakata tamaa na uongozi wenu ni kukamata huyu mtu jamani na sio kumlinda,waachieni basi wale wanaoshukiwa kule magerezani ili mufanye uchunguzi wakiwa nje nao,PUMBAVU na sera zenu za kinyonyaji...
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 17998 registered
female 4519 female
male 13396 male
month 77 new this month
New: blackbross
Who's Online Now
We have 56 guests online and 9 members online
BAYROS Geoff carine T_pain_Msomali Friiday TANAGWA MIPANGO hegga ferladha
2006-2007 © Copyright Bongo5.com