SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register





50 Cent aiteka Bongo PDF Print E-mail
Monday, 05 May 2008

50 Cent live

 

[Bofya hapa kuangalia video za 50 Cent live ndani ya Diamond Jubilee]

 

Saa nne na nusu juu ya alama 50 Cent alilivamia jukwaa la Diamond Jubelee akiwa na machizi wake wawili ambao ni Tony Yayo na Lloyd Banks, wote wakiwa wenye uchangamfu wa hali ya juu na kuifanya sura ya mchezo kuwa na mabadiliko, kwani kila mshabiki alishindwa kuvumilia kwa kubaki kwenye kiti na badala yake alisimama na Yowe zilizoambatana na kile 50 alichokuwa akiimba zilisikika kwa sauti za juu ile mbaya.


Idadi kubwa ya mashabiki iliweza kuoneka maeneo ya Diamond Jubelee kuanzia nyakati za saa Kumi jioni mpaka ulipofika muda wa show, wasanii kama Joh Makini, Chidi Benz, TMK Wanaume Halisi na TMK Wanaume pamoja na vikundi kadhaa vya utamaduni viliweza kufanya maonesho mafupi ya utangulizi kabla ya 50 kupanda jukwaani.


Baada ya 50 Cent kupanda Jukwaani hali ilikuwa inazidi kuwa tofauti kila dakika iliyokuwa ikiendelea kwenye show, kila baada ya muda alikuwa akizama ndani na kutoka akiwa amebadili t-shirt, pia kivutio zaidi siku hiyo ilikuwa ni mpangilio mzuri wa ngoma zake kwani kila iliyopigwa ilikuwa ni kali zaidi ya iliyotangulia, jambo ambalo lilikuwa likiwachizisha sana mashabiki waliohudhuria ukumbini humo.


Ngoma kama Ayo Technology, Candy shop, Straight to The Bank, In Da Club P.I.M.P, Get In To My Car, If I Cant, Follow My Lead, Pop Them Thang, Outta Control, Sensual Seduction, I get Money na mikono mingine kibao, ilionekana kumdatisha kila aliyehudhuria kwenye onesho hilo, halikadhalika alikuwa akirusha vivazi vyake kwa mashabiki ikiwemo vitu kama Kofia, T-shirt na viatu ikiwa ni ishara ya kuthamini uwepo wao na kumkubali.


Kwa Ujumla Show ilikuwa ni nzuri na yenye kuvutia sana, na unaweza kuona jinsi ambavyo uongozi mzima wa Clouds Entertainment ukiwa chini ya usimamizi wa wadhamini wakuu ambao ni kampuni inayotoa huduma ya simu za mkononi TIGO walivyoshirikiana na kuweza kulifanikisha hilo ambalo limekuwa ni kama surprise kubwa kwa wananchi na wapenzi wa burudani.

 

[Bofya hapa kuangalia video za 50 Cent live ndani ya Diamond Jubilee]

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
Comments
NewSearch
sonia - mamamia Tue, 06th May 08 - 08:57 am
BAHHHHH BAYAAAAAAAAAAAAAA
Mwajei Wed, 07th May 08 - 01:28 am
damnn!!! dat nigger z jst :kiss: wow!!
hanna - wowww! Wed, 07th May 08 - 07:42 am
haya wee 50 shilingi nakuaminia but ulitaka kuwaua ndugu zetu na sweta lako hah hah hah :woohoo: :woohoo: :woohoo: :woohoo: :woohoo: karibu tena ;)
gift2294 - g-unit Sat, 10th May 08 - 01:08 am
ye GGG G-unit so :angry:
Only registered users can write comments!

 
< Prev   Next >
Total Members
total 17998 registered
female 4519 female
male 13396 male
month 77 new this month
New: blackbross
Who's Online Now
We have 48 guests online and 9 members online
BAYROS Geoff carine T_pain_Msomali Friiday TANAGWA MIPANGO hegga ferladha
2006-2007 © Copyright Bongo5.com