SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Mambo ya Nje yataka kulipana posho za Sh300,000 kwa mwezi PDF Print E-mail
Wednesday, 30 April 2008

Waandishi Wa Mwananchi, Dar na Tanga

WAKATI walimu wakiishinikiza serikali iwalipe malimbizo ya fedha wanazodai, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeanza mkakati wa kuboresha maslahi ya watumishi wake, kwa kupendekeza kuwa kila mmoja alipwe posho ya Sh300,000 kwa mwezi kwa kufanya kazi saa za ziada.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaitafa, Balozi Seif Ali Idd wakati akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, uliofanyika katika Hoteli ya Mkonge, Jijini hapa.

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Bernard Membe, Naibu waziri huyo alisema uongozi umeamua kutoa kiwango hicho cha posho kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake.

Alisema kwa kuzingatia unyeti na uzito wa majukumu ambayo yamekuwa yakiwakabili watumishi wa wizara hiyo, ni wazi kuwa wanahitaji motisha katika ufanyaji kazi wao ili kuboresha ufanisi kwani kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifanya kazi nyingi katika masaa ya ziada bila kulipwa chochote.

Naibu Waziri huyo alisema utekelezaji wa mipango ya ulipaji wa kiwango hicho cha posho umepangwa kuanza mara moja ifikapo mwaka mpya wa fedha wa 2008/2009 ikiwa bajeti iliyoandaliwa itapitishwa kama ilivyopangwa.

�Katika bajeti wa wizara kwa mwaka ujao wa fedha tumeomba kila mfanyakazi alipwe Sh 300,000 kama posho ya kufanya kazi saa ya ziada kila mwezi, endapo bajeti yetu itapita kama tulivyoomba, utekelezaji utaanza mara moja,� alisema Idd.

Kwa upande wa kuwaendeleza kitaaluma, alisema pamoja na uchache wa watumishi, Wizara hiyo itaendelea kutafuta na kutoa fursa za masomo kwa ajili ya wafanyakazi wa kada mbalimbali ikiwamo maafisa wake kuhudhuria kozi mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Chama cha Walimu (CWT) kimesema kimeahirisha mgomo wao uliokuwa ufanyike Mei Mosi mwaka huu ili kutoa nafasi kwa serikali na chama kuhakiki madeni ya walimu.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jijini Dar es Salaam jana walifikia hatua hiyo baada ya kukutana na serikali na kwamba wamekubaliana madeni yote yahakikiwe na kwamba serikali ihakikishe yanalipwa ndani ya mwaka huu.

Katika kikao hicho pande zote mbili zilikubaliana kuanza zoezi la kuhakiki madeni ya walimu wanaohudumiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi litaanza wiki mbili kuanzia tarehe ya makubaliano yao.

Alisema katika kikao hicho waligundua kuwa kuna madeni mapya ambayo hayajalipwa, hivyo zoezi hilo liendelee kwa kuwashirikisha viongozi wa CWT ngazi ya wilaya na kwa kuzingatia kwamba serikali imeonesha jitihada za kulipa madeni ambayo yalishahakikiwa, huku ikiendelea kuhakiki madeni ya zamani yaliyosahaulika.

�Tumeamua kusitisha mgomo huo mpaka Julai 21 mwaka huu ili kuipa serikali nafasi ya kuendelea kuhakiki madeni yaliyosahaulika katika uhakiki wa Februari mwaka jana na ifikapo Julai 21 mwaka huu kama hawatalipwa tutaitisha mgomo upya,� alisema Mukoba.

Alisema katika kikao hicho walikubaliana kuwa zoezi la kuhakiki madeni ya walimu wanaohudumiwa na wizara, yataanza mwanzoni mwa mwezi ujao.

Alisema Mei 19, mwaka huu, walimu kupitia vyama vyao, watapiga kura ya kuunga mkono mgomo nchi nzima endapo madai mapya ya walimu hayatalipwa hadi Julai 21, mwaka huu.

�Tunajipanga vizuri zaidi ili mambo yakienda mrama tugome na mgomo hauna madhara yoyote kwa watumishi na tunawataka wasiogope vitisho vyovyote kutoka kwa mwajiri,� alisema Mukoba.

Rais huyo wa CWT alisema malipo yanayolipwa na serikali ni sehemu ndogo ya madai ya walimu, ambao mpaka sasa wanaidai serikali.

Alisema mapungufu mengi yalijitokeza wakati wa zoezi la kuwalipa walimu, kama vile malipo kwenda kwa watu wasio walimu na walimu kulipwa fedha pungufu na zilizohakikiwa.

Imeandaliwa na Jackson Odoyo, Emmanuel Mtinangi, Nora Damian na Burhani Yakub, Tanga

 

Source: Mwananchi

Comments
Search
Only registered users can write comments!

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 
< Prev   Next >
Total Members
total 21216 registered
female 5270 female
male 15866 male
month 21 new this month
New: Hapines
Who's Online Now
We have 37 guests online and 14 members online
swejacky Amiry debra kaga haywire preeety Tito Chamillionaire Danielita jeny2 Jozeedaking Tukwa kelly31 Hapines
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com