SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Wanazuoni watumie Lugha ya Kiswahili - Mkuchika PDF Print E-mail
Thursday, 24 April 2008

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amewaonya wanazuoni mahiri wa lugha ya Kiswahili na maprofesa kwamba, iwapo lugha za Kiafrika hazitaandikwa zitakuwa katika hatari ya kufa hivyo ni vema kuzikomalia lugha zetu.


Akifungua kongamano la maprofesa kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuhusu lugha katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ACALAN), Mkuchika alisikitishwa kuona nchi za Ulaya zinavyozidi kuzienzi lugha zao lakini Afrika hali ni tofauti watu wanaona aibu kutumia lugha zao na kujidai kwa kutumia lugha zizizo za kwao.


"Vita ya lugha ni ya muda mrefu, kama ninyi wataalam wa lugha mtashindwa kusaidia kukuza lugha zetu, kuziandika, basi hazitkuwa na uhai mrefu na zitakufa haraka," alionya Mkuchika.


Alisema wakati nchi za Ulaya zimefanya mapinduzi ya kujikwamua kiasi cha Kiingereza kuwa lugha kuu ya dunia, bado nchi za Kiafrika hazijiamini kuwa lugha zao zinaweza kuiga mapinduzi hayo.


Alifafanua kwamba, lugha za Kiafrika zinazovuka mipaka ziwe zinazungumzwa na makabila mbalimbali au zinatumiwa na jamii moja, ni vyombo muhimu vya kuunganisha watu ambao wametenganishwa na ukoloni.


"unaweza kuona nchi ndogo kama Iceland inaweza kutumia lugha zake hadi Chuo Kikuu kwenye mambo ya elimu, nchi nyingi za Kiafrika hata zile zenye watu zaidi ya 100 milioni, bado hazijifikirii kutumia lugha zao katika masuala kama hayo, ni jambo la kulifanyia kazi" alisisitiza.

 

 

Comments
Search
GAUCHO {space} {title} Thu, 24th Apr 08 - 04:51 pm
ni kweli kapteni mkuchika umeongea,ha2na budi kukikuza lugha ye2 ya taifa
kiswahili japo wanadai cc ni bado taifa changa,lkn kuna haja ya kuiendeleza
lugha hii kuanzia chekechea hadi vyuo vya elimu ya juu,mana ni 1 ya tamaduni ye2
ha2na budi kudumisha na kujivuna,ni vyema sana kuitangaza na kuitukuza lugha
hususan mpk nchi za mbali,ni lugha kubwa kiswahili lazima tujivunie lugha
ye2,tuache kasumba ya kutukuza sana lugha za kigeni na kuona ndio kama
usomiukiongea mbele ya kadamnasi unaonekana umesoma la!
Big Mic {space} {title} Fri, 25th Apr 08 - 01:02 pm
bwana gaucho hapo kuna utata kidogo kuhusu matumizi ya kiswahili vyuoni,mi
nadhani kiswahili kitumike mitaani kwasababu lugha hii bado changa sana kutumika
katika mitaala ya elimu ya juu,lakini pia uilimwengu sasa hivi ni kama
kijiji,tunawasiliana na watu wa mataifa ya mbali ndani ya siku dakika moja,na
lugha kuu itumikayo ni english,kwa hiyo tunafikiria kutumia hii lugha katika
elimu ya juu,jua kuwa itaathiri maeneo mengi sana,tutapata wasomi ambao ni
wazuri kwa lugha ya kswahili lakini wabababishaji wa lugha ya kiingereza,hawa
wasomi watasiliana vipi na wasomi wenzao wa nchi zingine?since hawajui kuongea
kiswahili?lakini si wasomi tu,hata wanamichezo na wasanii
wataathirika,chukulieni mfano mashindano ya POP IDOL,lugha inawaangusha sana
watanzania wengi,na hii ni kwasababu watanzania hatuna utamaduni wa kujinza
kukitumia kiingereza,kwakweli kukifanya kiswahili kuwa lugha yenye nguvu zaidi
ya lugha nyingine hasa katika maeneo ya elimu,tutasababisha kujitenga wenyewe
kiutamaduni na kiuchumi.tuongee kiswahili lakini sio katika njia ambayo wasomi
wengi wanashauri,sio wazuri kabisa.tupo katika dunia ya utanda
wazi,tunabadilishana habari,mawazo,tunafanya biashara,tunaweka appointment na
watu wa mataifa ya nje kupitia internet,na lugha kuu ni ENGLISH,hebu fikiria
kuhusu hilo,kiswahili sio lugha maarufu kama SPANISH or GERMAN or
FRENCH,tutafanyaje shughuri zetu kupitia internet hasa tunapotaka kuwasiliana na
international patners?
Only registered users can write comments!

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 
< Prev   Next >
Total Members
total 21216 registered
female 5270 female
male 15866 male
month 21 new this month
New: Hapines
Who's Online Now
We have 52 guests online and 17 members online
swejacky Amiry QEEN Flojoma debra kaga haywire preeety ommy name kanana Chamillionaire nanginyi jeny2 Jozeedaking Tukwa kelly31 Hapines
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com