SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

JK awakutanisha viongozi kuijadili Zimbabwe PDF Print E-mail
Friday, 18 April 2008

Rais Jakaya Kikwete

 

Na Mwandishi Maalum, New York

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, amekutana na viongozi mbalimbali duniani kujadili masuala makubwa likiwepo la Zimbabwe na kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Machi 29 mwaka huu.

Siku 20 zimepita tangu Zimbabwe ilipofanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge.

Katika mkutano wa awali uliotangulia mwingine wa masuala ya migogoro ya Afrika, Rais alikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown na suala la Zimbabwe ndilo lililotawala mkutano huo wa nusu saa.

Na katika hatua nyingine Mwenyekiti AU ametoa changamoto kadhaa kwa Umoja wa Mataifa (UN) za kuongeza mahusiano yake na AU , ili kwa pamoja vyombo hivyo vifanikiwe kutatua migogoro ya Afrika.

Rais Kikwete alitoa mapendekezo hayo mahsusi wakati anahutubia kikao maalum cha ngazi ya juu cha pamoja kati ya Baraza la Usalama la UN na Baraza la Amani na Usalama la AU.

Akizungumza mjini New York Marekani juzi, Rais alisema kuna umuhimu wa taasisi hizo mbili kuweka utaratibu wa jinsi UN inavyoweza kuingilia migogoro ya Afrika bila kusababisha mgongano na AU.

Kikao hicho kilikuwa kinatafuta njia za jinsi taasisi hizo zinavyoweza kushirikiana katika kutatua migogoro ya kisiasa ya Afrika.

Alisema kuna wakati AU inaona umuhimu wa kuingilia haraka na kumaliza tatizo katika nchi ya Afrika na inafanya hivyo, hata kama wajibu mkuu wa kumaliza migogoro duniani ni wajibu wa UN.

Alisema hilo linaweza kusababisha mgongano kati yake na AU kama halikuwekewa taratibu na mipaka inayojulikana na kukubaliwa na kila taasisi na UN na kuendeshwa na taasisi za kikanda kama AU, kugharimiwa na UN.

Kwa sasa taratibu za UN hairuhusu Umoja huo kugharimia shughuli hizo, hata kama zimeidhinishwa na Baraza la Usalama la UN.

Kikao hicho cha aina yake kimeitishwa na Afrika Kusini ambayo ndiyo Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la UN kwa mwezi huu.

Rais Kikwete pia alikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Jendayi Fraser, suala kubwa katika mkutano huo lilikuwa ni hali ya Zimbabwe na jinsi AU na Marekani zinavyoweza kuchangia katika kuhakikisha uchaguzi katika nchi hiyo unakamilika na kutangazwa matokeo ya urais.

 

Source: Nipashe

Comments
Search
Msambaa {space} {title} Sat, 19th Apr 08 - 01:43 pm
Yale yale, ya nyani kucheka ya wenzake, tunakimbilia kusuluhisha Kenya na
Zimbabwe wakati hapo karibu ng,ambo ya bahari yanatushinda? Zanzibar watapata
usuluhishi lini?
CATHBERT {space} i blv in Mugabe Mon, 21st Apr 08 - 01:49 pm
y sort out their issues after British takin over there land and makin the
citizens work for them psyin them less than minimum wage and makin lots of
profits here in uk.its tym they fight for is theres, so lets step out.
Msambaa {space} {title} Mon, 21st Apr 08 - 04:50 pm
Cathebert unasema I believe in Mugabe!?

U must be a blind man to believe in
Mugabe, really.
GAUCHO {space} {title} Mon, 21st Apr 08 - 05:53 pm
issue ya mugabe ni ya kisiasa sana,yule kajua kisiasa ngoja apate umaarufu kwa
kufanya vile,lkn ukweli ni kwamba kiuchumi hali ni mbaya zimbabwe na wa2
wanahangaika,sasa sisi tunaangalia usiasa na kumsifu kumuona kama anatetea ngozi
au rangi ye2 waafrika lkn ukweli wa mambo wengio we2 cc tulio nje ya zimbwabwe
hatuujui ni siasa tu kila m2 anaongelea lkn ukipata wa2 wa zimbabwe kuwasikiliza
ndio utapata ukweli,khs viongozi wa afrika na issue ya zimbabwe wote wana tabia
sawa hivyo kama kulindana mana kuharibu ni kawaida walio madarakani,kisha
wanapewa hifadhi nchi jirani eg taylor liberia alipopewa hifadhi nigeria,au
mengistu alivyopewa hifadhi zimbabwe.
Only registered users can write comments!

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 
< Prev   Next >
Total Members
total 21216 registered
female 5270 female
male 15866 male
month 21 new this month
New: Hapines
Who's Online Now
We have 38 guests online and 13 members online
swejacky Amiry said salehe debra moody x Tito Chamillionaire Danielita Jozeedaking kindgirl Tukwa kelly31 Hapines
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com