SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register

Wanandoa wapigwa mawe hadi kufa PDF Print E-mail
Tuesday, 08 April 2008
Na Kibuka Prudence, PST Kagera

Wanandoa wameuawa kikatili kwa kupigwa mawe na kuchapwa viboko hadi kufa huku wakiwa wamefungwa kamba na wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Bw. George Mayunga, alisema mauaji hayo yalitokea katika kijiji cha Lutunguru kitongoji cha Kilela, saa saba mchana ambapo wanandoa hao walivamiwa na kupigwa mawe na kikundi cha wananchi hao.

Bw. Mayunga, aliwataja marehemu hao kuwa ni Bw. Koronely Mboyerwa (69) na mke wake, Bi. Josephina Kolonery (56).

Alisema kabla ya mauaji hayo ya kikatili, kundi hilo lilifika nyumbani kwa Bw. Mbeyerwa na kuwafunga kamba na kuanza kufyeka shamba la migomba na kubomoa nyumba yao upande mmoja na kisha kuchoma vitu mbalimbali kama magodoro na vyakula.

Baadaye wananchi hao waliwachukua na kuwapeleka eneo la Kilela katika barabara ya Kaisho kwenda Mulongo na kuanza kuwashambulia kwa mawe na kuwapiga kwa fimbo hadi walipofariki dunia.

Kamanda aliiambia PST kuwa hadi sasa watu saba wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Kuraish Rwabitenga (36), Jumanne Cyprian (25), Focus Barnabas (48), ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji Rugalama, Theobard Thomas (45) na Augustino Batromeho (46).

Wengine ni John Simon (33), ambaye pia ni Mwenyekiti wa kitongoji Omumabale na Renatus Selestine (31), wote wakazi wa Kaisho wilayani Karagwe.

Bw. Mayunga alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

 

Source: Nipashe

Comments
Search
ghettoprince {space} lol Wed, 09th Apr 08 - 12:06 am
imani za kishirikina tu.. itakuwa...?!!
aki {space} duh...! Wed, 09th Apr 08 - 08:15 am
nilikuwa na hamu ya kujua sababu iliyowafanya wafanyiwe hivyo lakini mtoa habari
akekosa kitu muhimu hicho.anyway,sijui ni uchungu gani wananchi hao wakaamua
kufanya hivyo! vipi kama wakiwakamata MAFISADI itakuwaje? kwanini wao ndio
wasifanyiwe hiyo kitu..tukianzia na hawa wa RIChArD wa MOndUli...!
Only registered users can write comments!

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Tag it:
Delicious
Furl it!
Spurl
NewsVine
Reddit
YahooMyWeb
Digg
blogmarks
feedmelinks
co.mments
 
< Prev   Next >
Total Members
total 21216 registered
female 5270 female
male 15866 male
month 21 new this month
New: Hapines
Who's Online Now
We have 50 guests online and 17 members online
swejacky Amiry QEEN Flojoma debra kaga haywire preeety kanana Chamillionaire Danielita nanginyi jeny2 Jozeedaking Tukwa kelly31 Hapines
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com