| TMK Wanaume wasambaratika |
|
|
|
|
Kutokana na hali hiyo unaweza kuchagua neno la kutumia kuhusu hali ilivyo ndani ya kundi hilo. Ama waweza kusema mambo yanakwenda segemnege, hobelahobela, hangahanga, msagunda, arijojo, shaghalabaghala au shelabela, yote yakimaanisha kwamba ni ovyoovyo, bila ya mpango maalumu au taratibu. Habari zilizopatikana ndani ya kundi hilo na kuthibitishwa na Meneja wake, Said Fela na baadhi ya wasanii ni kuwa mambo sasa si shwari. Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kwamba mmoja wa waasisi wa kundi hilo, Juma Kassim 'Sir Nature' amejiengua kinyemela na wasanii wengine watatu. "TMK Wanaume mambo hayapo vizuri, inasikitisha kuona wasanii wamegawanyika ikiwa ni miezi michache tangu kundi lisherehekee kutimiza miaka minne tangu lianzishwe. "Lakini ndio maisha, Nature amejiondoa, lakini vichwa vingine bado vipo na vina nguvu ya kuendeleza makamuzi, watu wanasonga mbele, shujaa halilii bunduki," kilisema chanzo chetu. Source: Bongo5 Error, missing joomlaboard config file! Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you'd like to share please send an email to This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it
Only registered users can write comments!
Powered by !JoomlaComment 3.26
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved." |
||||||
| < Prev | Next > |
|---|








