Burudani

Conscious Hip Hop 10 bora za Tanzania mwaka 2012

By  | 

Hizi ni nyimbo 10 bora za conscious Hip Hop kutoka Tanzania zilizofanya vizuri zaidi mwaka 2012 kwa mujibu wa Bongo5.

Kala Jeremiah – Dear God

Dear God iliyotengenezwa na D Classic imetoka mwezi September mwaka huu lakini tangu itoke mpaka leo haiwezi kupita siku bila kusikia ikichezwa redioni. Ni wimbo ambao mashabiki wa Hip Hop wameugeuza Sala. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtangazaji wa Clouds FM, B12 kuhusu nyimbo iliyokubalika zaidi mwaka huu, Dear God umekamata nafasi ya kwanza kwa upande wa Hip Hop. Ni wimbo ambao umemrudisha tena Kala kwenye ramani baada ya kupotea kwa muda.

Fid Q ft Yvonne Mwale – Sihitaji Marafiki

Ngoma hii iliyotengenezwa na J Ryder ilikuwa ni single ya pili kutoka kwenye albam ijayo ya Fid iitwayo Kitaalojia. Fid aliamua kumshirikisha mzambia Yvonne Mwale aliyeipamba ngoma hiyo kwa kiitikio kitamu. Sihitaji Marafiki ilikuwa ni ngoma iliyodhihirisha tena uwezo mkubwa wa kiuandishi aliojaaliwa rapper huyu ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda.

Darassa ft Winnie – Nishike Mkono

Nishike Mkono ni ngoma iliyotengenezwa na Manecky ambaye pia alitengeneza single mbili za mwanzo za Darassa. Hivi karibuni Darassa aliongea na Bongo5 na kusema kuwa mtaa ndio humuinspire kuandika nyimbo zake. “Mimi niko mtaani na kuna vitu vyote hivi, maisha yetu sisi yako huko tunafanya kwaajili ya watu wa mtaani. Mtaani kuna mambo mengi na kati ya vitu ambavyo viko mtaani hakuna good times. Hakuna good life hiyo ambayo labda kuna watu wengine wanaishi,”alisema Darassa.

“Kwahiyo mimi najaribu kuandika maisha halisi ambayo nakutana nayo mtaani na watu wa karibu ambao naishi nao, pengine inaweza kuwa sio mimi tu kwasababu mimi siwezi kuwa na shida kila siku, najaribu kuangalia maisha ya watu wengi nayafanyia nyimbo na vitu kama hivyo.”

Stamina ft Jux – Alisema

Stamina ni rapper kutoka Morogoro ambaye mwaka 2012 amejichukulia sifa kubwa katikia uandishi bora wa mistari na performance zake zenye nguvu stejini. Alisema ni wimbo unaozungumzia ushauri muhimu kutoka kwa marehemu mama yake.

Jos Mtambo ft. Belle 9 – Naongea na Roho

Naongea na Roho ni ngoma iliyotayarishwa na J Ryder wa Tongwe Records. Katika ngoma hii Jos Mtambo anawakumbuka watu muhimu katika tasnia ya burudani waliotangulia mbele za haki.

Mwana FA ft. AY na Dully Sykes – Ameen

Pamoja na kuleta maneno ya hapa na pale kuwa Duly Sykes alisample wimbo wa Cecile kutengeneza ngoma hii, Ameen ni track yaFA iliyojadiliwa na kusifiwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ni wimbo wa kumuomba mwenyezi Mungu akujaalie mambo mema zaidi duniani.

Chidi Benz ft. Ben Pol- Nipokee

Huu ni wimbo wa kutubu zaidi kwa mwenyezi Mungu baada ya kufanya dhambi nyingi. Pamoja na mashairi mazuri na beat kali, Nipokee umebarikiwa kuwa na chorus tamu kutoka kwa mkali Ben Pol.

G Nako ft Nikki wa Pili – Bado Ngware

Hapa Fundi Samweli alijipinda hasa kutengeneza beat ya wimbo huu. Ni ngumu kufikiria haraka haraka kuwa ngoma hii imetengenezwa Tanzania. Bado Ngwale maana yake ni ‘Bado Mapema’ na mashairi yake yana kila sababu za kukupa matumaini ya kuendelea kupambana na maisha. Ngoma hii ina chorus tamu sana.

Izzo B – Mwaka Jana

Mwaka Jana ni ngoma iliyotengenezwa na Manecky. Izzo aliutumia wimbo huu kuelezea jinsi alivyouchukua mwaka 2011.

Suma Mnazaleti ft Mabeste na Ben Pol – Tafakari

Suma Mnazaleti ni rapper mwenye sauti ya tofauti pengine kuliko wasanii wote wa Hip Hop nchini. Ana kijisauti kidogo hivi ambacho uwezo wake kiuandishi huwafanya watu wasikizingatie sana udhaifu wake. Katika tafakari, Mabeste pia anasikika na mashairi yake.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments