Wahariri Nao Wajibu Mapigo
Wahariri wa vyombo vya habari nchini, wameamua kwa pamoja kususia kuandika habari zote zinazomhusu waziri huyo kupinga hatua yake ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi kutochapishwa kwa miezi mitatu.
Simba Yaifunga Kagera BAADA ya kugubikwa mgogoro mkubwa, Simba imeweka kando na kujipoza machungu hayo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mbaya wa Yanga, Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nguza Na Wanawe Waimba GerezaniMwanamuziki Nguza Viking na mwanae Papii Kocha waliwapagawisha kwa burudani safi ya muziki wafungwa wa gereza la Ukonga katika bonanza lililofanyika jana katika viwanja vya Magereza, Ukonga.
Kawawa Kuongoza Kumbuku Ya NyerereMlezi wa chama cha michezo ya jadi mkoa wa Dar Es Salaam ambaye pia ni makamu wa pili wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu Mh.Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita),atawaongoza waaalikwa mbalimbali,wapenzi na washabiki wa mchezo wa bao katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere(Saba Saba ) barabara ya Kilwa kukumbuka miaka 9 ya kifo cha mwasisi na Baba wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Tamasha La Filamu Laanza Rasmi Tamasha la Filamu za Ulaya European Film Festival limeanza rasmi kuonyesha filamu siku ya ijumaa katika ukumbi wa New World Cinema.