SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register
Bongo5 Forum
Welcome, Guest
Please Login or Register.
Lost Password?
_GEN_GOTOBOTTOM Post Reply

TOPIC: Re:JK

#2552
aki (User)
Fresh Boarder
Posts: 2
graphgraph
Click here to see the profile of this user
Re:JK 2008/01/21 19:09  
mmh..maneno yamenichoma! maana inji kukosa lumeme tena? uwii!! na yeye kuna kona kila siku,inagawa alikuwa wathiri wa mambo ya inji za inje,kila siku alikuwa hakai bongo,bado anapenda tu kwenda inje ya inji..uwiii~!mapesa ya BOT,madini na mambo kama hayo yote anayafanya kiushikaji..aisei! baraka ya kwenda inje na kupiga picha na nyota wa miziki,eti ndio laisi wa Bongo.yaani inji ina kila kitu,lakini masikini...sasa kama tuna madini aina zote mfano TANZANITE(inapatikana bongo tu,hakuna sehemu nyingine duniani)bandari zisizopungua 6,mbuga za wanyama,mlima kilimanjaro na vitu kibao vinavyoweza kutupa utajiri lakini bado ni masikini,na prezidenti hajui kujipanga ili tuondokane na umasikini..uwiii! nisije kupandisha mori mie~!naona kuna haja kabisaa ya kufikiria upya..dawa ni kuwanyima hawa ma sisiemu hiyo 2010 basi tuone na wengine wana hasira gani za maendeleo ya bongo.
  The administrator has disabled public write access.
#2553
ghettoprince (User)
Fresh Boarder
Posts: 15
graphgraph
Click here to see the profile of this user
Re:JK/ KUNANI IKULU?????? 2008/01/22 07:10  
dah.. mi naona tumuache homboy atafanyanini tena... si nimesikia kuna fagio analipitisha.. BOT ..!!! ila najiuliza kwa nini atangaze kumfuta kazi .. balali akiwa nje ya nchi... jamaa si anaweza akakimbia... loooo!!! jamaan hivi kunani pale ikulu...!!!..? mbona mambo kimya kimya.. nliposikia ya mabilioni ya pesa yaliopotea kwa ajili ya kampuni hewa.. walah roho iliniuma.. mkapa naye alipokopa fedha nyingi wakati akiwa RAIS NA AKZIRUDISHA KWA kipidi kifuPI tU..?.. nafikiri balali hayupo peke yaKE yale mabilioni.. HEBU NKAYE KIMYA .. nsijE nika...... tumpe mda muheshimiwa kikwete naona ameanza kazi..
  The administrator has disabled public write access.
#2555
Yassern (User)
Fresh Boarder
Posts: 10
graphgraph
Click here to see the profile of this user
Re:JK/ KUNANI IKULU?????? 2008/01/23 10:57  
mmh..kaka ,unajua Homeboy alichaguliwa kwa kura nyingi mno,wenyewe waliita kwa "kishindo" na kumbuka aliahidi mambo mengi makubwa.vijana kwa wazee,(na hata wapinzani baadhi yao)walimpa kura wakitegemea,au tukitegemea kuwa Bongo maisha yatakuwa bab kubwa..duh..mzee kumbe sasa zile ni sawa na ahadi za "ndio mzee" kwenye nyimbo ya Pro.J maana maisha yanazidi kuwa magumu mno hasa kwa mtu wa kipato cha chini.embu tuanglie tu ni kitu gani ambacho mpaka sasa kime kaa mwake? ukweli utaona hakuna..labda UFISADI,MIKATABA MiBOFU,AJALI,KUBEBANA NA KUONEANA AIBUna mambo kama hayo bila kusahau baba yao RUSHWA.mkuu,ninakwambia safari hii,"sio mzee" itatawala kwenye uchaguzi ujao,maana watu wamechoooka! kwa kumalizia tu,ikulu,kwa marais wetu wa kiafrika,hususani bongo,ni sehemu ya kunyoosha miguu na kumaliza zile ndoto walizokuwa nazo,kwani sheria(KATIBA)ya nchi haimbani rais kufanya kinyume na urais wake,kwani yeye ni final say wa kila kitu.basi bongo ndio inateketea mkuu..baraka ya kuwa na kila kitu cha kutuwezesha kuwa maTAJIRI angalau katika nchi za kiafrika lakini hatuna UONGOZI..tendo la kuwa na vitu kama walivyosema wakubwa hapa,mfano madini(tanzanite,diamonds,Gold etc),bandari,mlima KILImanjaro,national parks nk.embu fikiria tu kama rais asingefanya world tour,pesa za Balali,mambo ya BUzwagi,na mengine meengi kama angekuwa mkali tungekuwa wapi bongo? hivi unajua kuwa tunasehemu nyiingi za kupata kodi hasa migodini,je unajua nani anaogoza bongo kwa kulipa kodi..eti KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) ndio inaongoza,kwanini wasiwe hao wanaoiba mali ya wabongo,yaani wanaovuna madini yetu? inasikitisha sana bongo.tena viongozi ndio akili hata moja hawana,kazi kuropokwa vitu vya ajabu,mfano wenye ngoma wawekewe alama,mara bucha zifungwe ziwepo supamaketi tu.nakwambia nimesoma points za watu mbali mbali,zinatia hasira mno..maana viongozi wote hawasikilizi lolote toka kwa wananchi.
  The administrator has disabled public write access.
#2557
Msambaa (User)
Fresh Boarder
Posts: 49
graphgraph
Click here to see the profile of this user
Re:JK 2008/01/24 20:54  
Nyingine!.



Slaa anyaka skendo lingine

2008-01-24 17:22:18
Na Job Ndomba, Jijini

Yule mbunge maarufu wa kulipua maskendo, Dokta Wilbroad Slaa (CHADEMA-Karatu) amenyaka skendo jingine bab`kubwa linalohusisha ulaji wa mabilioni kibao ya pesa za walalahoi.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Dk.Slaa amesema pesa hizo zilizoliwa na vigogo ni kutoka katika mfuko wa Import Support uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Japan.

Amesema mfuko huo uliokuwa na mabilioni kibao ulilenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogo, lakini mapesa hayo yakaliwa hivi hivi na vigogo baada ya kukopeshana na kushindwa kulipa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, mfuko huo sasa umefutwa baada ya kugundulika umetumiwa vibaya na vigogo hao anaodai, wengi wao walifungua makampuni hewa kwa ajili ya kukamilisha ulaji wao.

``Vita dhidi ya ufisadi haijaisha, kwani baada ya hili la BoT najiandaa kulipua hili la upotevu wa mabilioni, kutoka katika mfuko wa Import Support,`` akasema Dk. Slaa.

Amesema nchi hii ina maskendo mengi sana yanayofanywa na vigogo na hivyo lazima wachache wajitolee kuwashitaki kwa wananchi kwa ajili kuokoa uchumi wa taifa.

``Unajua tunapowataja mafisadi hawa, wananchi wanatakiwa watuunge mkono kwa kuwa kuna mapesa kibao yameibwa na vigogo,`` akaongeza.

Amesema mfuko wa Import Support ulianzishwa kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, lakini wakapigwa changa la macho na mapesa hayo kuwafaidisha vigogo wachache.

Hata hivyo Dk. Slaa hakutaka kutaja ni lini atalipua bomu hilo, lakini amesisitiza kuwa yuko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha uchunguzi wake.

``Kwa sasa siwezi kukuambia ni lini nitalipua ila wakati ukifika, nitawasilisha madai yangu mahali husika kama ilivyokuwa kwa lile skendo ya BoT, licha ya kwamba baadhi ya watu walianza kunibeza,`` akasema.

Dk. Slaa ndiye aliyeibua skendo la BoT Julai mwaka jana, katika kikao cha Bunge wakati Waziri wa Fedha Bi.Zakhia Meghji akiwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya wizara hiyo.

Hata hivyo baada ya kuibua hilo, Dk. Slaa alitakiwa kutoa hoja binafsi ambapo pia aliamua kushitaki kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara pale Mwembeyanga, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya matokeo ya skendo la Benki Kuu ni kubainika kwa ulaji wa zaidi ya shilingi bilioni 133 na kutimuliwa kazi kwa aliyekuwa gavana wa taasisi hiyo, Dk. Daud Balali.

* SOURCE: Alasiri
  The administrator has disabled public write access.
_GEN_GOTOTOP Post Reply
© Copyright 2007 Best of Joomla, Powered by FireBoardget the latest posts directly to your desktop
Total Members
total 21205 registered
female 5268 female
male 15857 male
month 10 new this month
New: glamour
Who's Online Now
We have 32 guests online and 8 members online
baiby yeah jahman Carmelo ThAnX fids.inc samirabeauty makaveli jr ERICK JOHN9
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com