|
Michango ya Fedha Kuzalisha na Kusambaza Umeme Tarafa ya Madaba Bw. Engelbert Mlelwa, Mwenyekiti Wilima,DSM Utangulizi: Wakazi wa Madaba tuna bahati ya pekee kwani mipango ya kupata umeme inakaribia sana kukamilika. Maneno haliwi haliwi sasa yatabadilika kuwa yamekuwa. Giza nene litatoweka kutokana na mwanga mkali. Hii ni hatua madhubuti kabisa ya kufikia lengo la dira ya Taifa 2025. Kwa hakika bahati hii sherti tuikamate. SIDA Hadi sasa SIDA imetumia zaidi ya Tshs 200,000,000/= kwa tafiti mbali mbali Tathimini ya mazingira Utafiti juu ya hali ya kiuchumi na kijamii katika tarafa Kuandikisha kampuni WETCO ( Wino Electricity and Telecommunication Company) Maandalizi ya Business Plan ya WETCO Uchambuzi na wataalam wengine wa kujitegemea kubaini iwapo mradi utafanikiwa au la Kimsingi mambo yote yamedhihirisha kuwa Mradi huu utafanikiwa Nini kina endelea sasa Ukamilishaji wa andiko kazi ambayo itakwisha kabla ya Desemba SIDA inategemewa kuukubali mradi huu ndani ya Desemba au mapema January 2004. MLH wamemleta mtaalam kutusaidia kupanga utekelezaji. Wengine watakuja. Masharti ya Mradi Mradi utagharimu Tshs 3,000,000,000/= Tunatakiwa kuchangia Tshs 300,000,000/=nusu, fedha taslimu na iliyobaki kwa kazi za mikono. Fedha taslimu italipwa Tshs 50,000,000/= kila mwaka kwa miaka mitatu. Malipo ya Tshs 50,000,000/=sherti yafanyike katika miezi sita kila mwaka toka siku ya mkataba vinginevyo mkataba unavunjwa.. Maamuzi ya Tarafa Kila mtu mzima mkazi wa Madaba achangie Tshs 4000 kila mwaka. Michango imeanza. Wazaliwa wa Madaba wanaoishi nje ya tarafa wachangie zaidi ya Tshs 20,000/=kwani wanaelewa faida za umeme, pia hawatashiriki kazi za mikono.Wasiojiweza watoe chochote wajisikie Kushiriki. Nani atapata umeme? Wanaochangia watapewa kipaumbele Wenye uwezo wa kuvuta umeme majumbani/biashara Wenye uwezo wa kulipia matumizi ya umeme Sehemu za umma kama zahanati, shule,makanisa,misikiti n.k. Utaratibu wa Malipo Au onana na Sigilada au Beatus Kinemo,waweka hazina, au Mwenyekiti au Katibu wa Wilima DSM au lipa moja kwa moja CRDB Songea Br. Wino SACCO AC 01J2085151600 na kutoa nakala ya risiti kwa mweka hazina moja wapo. Weka Historia ya Tarafa Yako, Changia Msingi wa Kudumu wa Maendeleo
|