VipimoNyama ya mbuzi 2 Lb (Ratili)
Thomu na tangawizi 1 Kijiko cha supu
Bamia Kiasi
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Vitunguu 2
Nyanya iliyokatwa katwa 4
Chumvi kiasi
Garam masala 1 Kijiko cha supu
Kotmiri ½ Kikombe
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Nyanya ya kopo 3 Vijiko vya supu
Ndimu 1
Mafuta ya kukaangia Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na KupikaChemsha nyama pamoja na chumvi, thomu na tangawizi, pilipili na kitunguu kwa maji ya kiasi.
Hakikisha nyama itakapowiva ibakie supu yake kidogo.
Katika sufuria weka mafuta yapate moto, kaanga vitunguu mpaka view rangi ya hudhurungi, tia thomu kaanga kidogo tu.
Kisha tia bizari, kotmiri na ukaange kidogo, tia nyanya kaanga zilainike halafu tia nyanya ya kopo.
Weka bamia na endelea kukaanga.
Mimina supu ya nyama, changanya kisha iwache kwenye moto kidogo kuwivisha bamia.
Tia ndimu kisha mimina katika bakuli na itakuwa tayari kuliwa.