SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register
Bongo5 Forum
Welcome, Guest
Please Login or Register.
Lost Password?
MAKARONI YA KUKU NA BASHAMEI (1 viewing)
_GEN_GOTOBOTTOM Post Reply

TOPIC: MAKARONI YA KUKU NA BASHAMEI

#2470
tatu (User)
Junior Boarder
Posts: 148
graphgraph
Click here to see the profile of this user
MAKARONI YA KUKU NA BASHAMEI 2007/11/13 14:54  
MAKARONI YA KUKU NA BASHAMEI

Makaroni (aina yoyote) 500 gms

KUKU:

Nyama ya kuku bila mafupa
iliyokatwa ndogo ndogo 1LB
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
chumvi kiasi


VIPIMO VYA SOS NYEUPE 'BASHAMEI'

Mafuta ya kupikia 1/4 kikombe
Nyanya – kata ndogo ndogo 4
Nyanya kopo 4 vijiko vya supu
Kechapu ya nyanya (tomato ketchup) 5 vijiko vya supu
Supu ya kuku ya vidonge
(chicken stock/Maggi cubes) 2 vidonge
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Viungo vya Kiitali ukipenda
(Italian spices; Oregano, mint, thyme) 1 kijiko cha supu

NAMNA YA KUTAYARISHA

1. Mtie kuku chumvi, pilipili manga, thomu, mpike awive. (Unaweza kutumia kidari au sehemu yoyote ya kuku, ukishaipika utoe mafupa na uchambue nyama ndogo ndogo)
2. Epua weka kando.
3.Tia mafuta katika sufuria, kaanga nyanya, tia nyanya kopo, kechapu, viungo vya kiitali, pilipilimanga , chumvi na kidonge cha supu (Maggi cube).
4. Pika hadi sosi iwe tayari isiwe nzito sana, ongeza maji 1/2 kikombe.

*VIPIMO VYA BASHAMEL NA NAMNA YA KUTAYARISHA

Unga mweupe 1/2 kikombe
Siagi (butter) 3 vijiko vya supu
Maziwa 2 vikombe vikubwa (mugs)
Kidonge cha supu (Maggi cube) 1

1. Tia unga katika sufuria.
2. Tia siagi kaanga kidogo ubadilike rangi unga uwe rangi ya hudhurungi hafifu. (light brown)
3. Tia maziwa koroga kwa mwiko wa kupigia mayai au tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage ili uondoshe madonge.
4. Tia kidonge cha supu (Maggi cube) kisha rudisha katika moto kidogo uipike sosi. Isiwe nzito sana iwe kama kastadi na kama nzito sana ongeza maziwa.

* Iwe kazi ya mwisho kutayarisha sosi, umwagie katika makoroni ukiwa tayari umeshapanga kila kitu.

VYA KUMWAGIA NDANI NA JUU YA MAKARONI

Jibini zote ziwe zimekunwa (grated)
Jibini ya cheddar (cheddar cheese) 200 – 250 gm
Jibini ya mazorella (mozorella cheese) 200 –250 gm

.UTAKUWA UMETAYARISHA VITU HIVI VIWE TAYARI

1- Kuku aliyepikwa na kuchambuliwa
2- Sosi ya nyanya
3- Makaroni yaliyochemshwa yakaiva
4- Sosi ya Bashamel
5- Jibini iliyokunwa (shredded cheese)

KUMALIZIA KUPIKA MAKARONI

1.Panga nusu makaroni katika bakuli au trea ya kupikia katika oveni.
2. Tia nusu ya sosi ya nyanya
3.Tia nusu ya kuku aliyechambuliwa
4. Tia nusu ya jibini iliyokunwa
5. Rudia kupanga tena kwa mpangilio huo huo.
6. Malizia kwa kumwagia sosi ya bashamel hakikisha inaingia pande zote na ndani ya makaroni.
7. Pambia kwa viungo vya kiitali au naanaa (mint) iliyokatwa ndogo ndogo.
8. Pika katika oveni moto wa 350-400º kwa muda wa dakika 15-20 hadi jibini sosi ya bashamel iwive.
9. Epua ikiwa tayari kuliwa.

Post edited by: tatu, at: 2007/11/13 13:00
  The administrator has disabled public write access.
_GEN_GOTOTOP Post Reply
© Copyright 2007 Best of Joomla, Powered by FireBoardget the latest posts directly to your desktop
Total Members
total 21206 registered
female 5268 female
male 15858 male
month 11 new this month
New: andyquicks
Who's Online Now
We have 48 guests online and 3 members online
Carmelo ThAnX ireland
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com