VIPIMO
Kunde 1 ? Vikombe
Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa ? Kikombe
Baking soda ? Kijiko cha chai
Masala 1 Kijiko cha chai
Maziwa 2 Vijiko vya supu
Chumvi 1 ? Vijiko vya chai
Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
-Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
-Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.
-Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
-Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
-Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
-Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
-Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo