SAMAKI -Samaki wa sea bass vipande 1 1/2 Lbs (Ratili)
-Thomu iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
-pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
-Bizari ya manjano au ya pilau 1/2 Kijiko cha chai
-Paprika ya unga au pilipili ya unga 1 kijiko cha chai
-Chumvi Kiasi
-Ndimu
-Mafut 3 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUPIKA -Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
-washa oven moto wa 400F.
-Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
-kishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA -Gwaru (green beans) 1 LB
-thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
-Karoti 4-5
-chumvi Kiasi
-Bizari ya manjano 1/2 Kijiko cha chai
-Pilipili manga 1/4 kijiko cha chai
-Mafuta ya zaituni Kiasi
NAMNA YA KUPIKA -Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
-Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru, halafu weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
-Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
-Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.
Imeandaliwa na Tatu.