|
I once discussed this somewhere else, but I am interested in soliciting your opinions.
Sisi tuliozaliwa Bongo, tunakua tukiongea kiswahili (na labda lugha ya kikabila). Tukianza shule, tunajifunza tukitumia kiswahili. Kale kadarasa ka kiingereza hakatufundishi lugha ya kiingereza. Baada ya kumaliza darasa la saba, tunaanza shule za sekondari, tukifundishwa kila masomo kutumia kiingereza. Wanafunzi bora waliofaulu darasa la saba kirahisi, wanafeli form IV vibaya. Hawa wanafunzi wa sekondari, wakiwa darasani wanaongea kiswahili, na pia wakitoka nje ya darasa. Kiingereza kinakuwa, ukweli ukitajwa, kigumu tu (kwa wengi, anyways).
Mimi nashangazwa sana kwa hivyo baada ya miaka mingi ya mtindo huu wa elimu, wataalamu hawajaamua kuwa 'tunaua' maendeleo ya mbeleni ya wanafunzi nchini mwetu. Yaani hawa wanafunzi hawaelewi wanachofundishwa shuleni (secondary), na wajanja wanategemea kutumia kumbukumbu kufaulu mitihani. Swali likibadilishwa, wanapotea kabisaa. Basi wakifaulu, wanaendelea na kusoma chuoni wakitumia kumbukumbu... Yaani kweli sisi tunategemea kushindana na nchi za Anglo-phone wakati tukielimika vyuoni? Ukweli ni kama sisi wabongo hatukuwa wajanja, na kujisomesha nje ya madarasa yetu - wengi tungeonekana ka ni wajinga vyuoni nchini na ulaya.
Sisi wabongo ni mabingwa wa kiswahili, kwa hiyo, ni maoni yangu kwamba hata tukianza kufundishwa primary school tukitumia kiingereza, tutakijua kiswahili kama tunavokijua siku hizi, kwa sababu, tutatumia lugha nje ya madarasa. Pia, tutakuwa wanafunzi bora ambao wanaweza kusoma popote duniani wanakotumia kiingereza.
Jamii, mnafikiriaje? Maoni yenu ni muhimu, na labda mtaungana nami ili tubadilishe huu mtindo wetu wa elimu.
It isn't about shedding our utamaduni, far from it, it is about giving us an equal competitive edge education-wise. I can only imagine how Tanzanians will fare given how intelligent we are when we understand 'what time it is'. Seen?
Peace bongo5 massive.
|