|
je una lolote ambalo Unaweza kukumbuka maisha ya miaka ilee ya shule za msingi. sababu ni kutaka tu kukumbushana Maisha ya shule ya msingi.vituko Vyote ,na jinsi tulivyo jifunza,ila tucheke na kufurahi pamoja.Mwaga hapa .mfano -jinsi ulivyokuwa unaruka dirisha kwa kumkimbia mwalimu wa kiinglishi, -jinsi ulivyokuwa hupendi kuoga, -jinsi ulivyokuwa mwizi wa madaftari ya wenzako, -jinsi ulivyokuwa fundi wa kuibia mitihani(kupiga chabo), -jinsi ulivyokuwa fundi wa kutumia nyenzo kwenye mitihani, -jinsi ulivyokuwa fundi wa kuandika barua kwa mademu, -jinsi ulivyokuwa mgomvi na wenzako, -jinsi ulivyokuwa muuzaji mzuri wa visheti,keki,bagia n.k za waalimi, -jinsi ulivyokuwa mzembe wa kitu fulani, -jinsi ulivyokuwa mtaalam wa kitu fulani, -jinsi ulivyokuwa unachukia siku ya usafi NA MAMBO MEENGI KAMA HAYO.leta nasi tufurahi mambo hayo,ila tutumie lugha safi ili tupende na kucheka pamoja kwani wengi tunaamini maisha ya shule ya msingi yalikuwa sawa na kuwa jeshini maana kila kitu tulikuwa tunataka kiwe kirahisi na mwishowe unajikuta unakula mboko(bakora)lakini hata hukomi,unatafuta njia nyingine. anza sasa ,tupe unachokumbuka...!
Post edited by: Yassern, at: 2008/06/20 04:14
|