Kawawa Kuongoza Kumbuku Ya NyerereMlezi wa chama cha michezo ya jadi mkoa wa Dar Es Salaam ambaye pia ni makamu wa pili wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu Mh.Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita),atawaongoza waaalikwa mbalimbali,wapenzi na washabiki wa mchezo wa bao katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere(Saba Saba ) barabara ya Kilwa kukumbuka miaka 9 ya kifo cha mwasisi na Baba wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Tamasha La Filamu Laanza Rasmi Tamasha la Filamu za Ulaya European Film Festival limeanza rasmi kuonyesha filamu siku ya ijumaa katika ukumbi wa New World Cinema.
Taifa Stars KiwangoBaada ya timu ya soka ya taifa, Taifa Stars juzi kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Cape Verde juzi, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Marcio Maximo amesema kuwa sasa anaamini kikosi chake kimekuwa bora.
Chadema, CCM Ngoma Nzito TarimeWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walikuwa wakishangilia kwenye mitaa mingi ya mjini Tarime, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya baada ya matokeo ya ubunge na udiwani kuanza kupatikana kutoka vituoni.
Taifa Kuivaa Cape Verde KeshoTimu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kesho inajitupa dimbani katika uwanja mkuu wa Taifa kupambana na timu ya taifa ya Cape Verde katika mpambano wa kukamilisha ratiba ya kugombania tiketi ya kombe la dunia na mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Afroka Kusini na Angola.