Gray Mgonja Naye KortiniKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, ambaye yuko katika likizo ya kustaafu, Grey Mgonja, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka manane.
Serikali Yala Sahani Moja Na RichmondSerikali imefungua uwanja mpya wa mapambano dhidi ya wabunge baada ya kutangaza wazi kwamba ina mpango wa kununua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans, uamuzi ambao unapingwa vikali na wawakilishi hao wa wananchi.
Pinda Acharukia Semina MashangingiHatimaye, Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha walipa kodi juu ya matumizi makubwa yasiyo ya lazima serikalini katika ununuzi wa magari ya kifahari maarufu kwa jina la mashangingi na sasa ununuzi wake utapunguzwa kwa kiwango kikubwa.
URA Yaiadhibu Mtibwa TuskerTIMU ya Mtibwa Sugar imeanza vibaya michuano ya Kombe la Tusker kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).
Stars Yapokelewa Kishujaa DarMaelfu ya mashabiki wa soka wa jijini Dar es Salaam jana walijitokeza katika mitaa mbalimbali ili kuilaki timu ya taifa, Taifa Stars iliyorejea nchini kutoka Sudan baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki fainali za kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN).