SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register




 

Results 61 - 90 of 2022
Rubani mkuu wa atc kepteni george mazula amefariki dunia nyumbani kwake mtaa wa nyumbu, mikocheni, dar leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kupumua.

Kijana Deus Mallya (27) anayedaiwa kuwa dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe wakati wa ajali, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakaimu Mkazi Dodoma, chini ya ulinzi mkali.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, almanusura kujeruhiwa kwa kurushiwa mawe na wengine wakitaka kumkata kwa mapanga lakini aliokolewa kwa juhudi za ziada.....

Mazishi ya Mh. Chacha Wangwe, aliyekuwa Mbunge wa Tarime aliyefariki dunia kwa ajali ya gari majuzi huko Dodoma, yameshindwa kufanyika jana kijijini kwake Kamokorere baada ya kufumuka kwa vurugu kubwa ambapo...

Ombaomba mkongwe na maarufu nchini, Anthony Matonya ametoroka kwenye kambini alikokuwa akitumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kosa la uzururaji na kuomba fedha bila sababu za msingi.

Wakazi watatu wa jijini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuiba gari lililokuwa limeegeshwa nje ya kanisa la Mt. Joseph na muumini Gregory Viscent (34), aliyekuwa amekwenda kusali.

Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Tumaini, huko maeneo ya Kurasini Sheila Wasukira (22), amekutwa amekufa chumbani kwa mpenzi wake baada ya kujinyonga kwa kutumia kitanzi cha kamba alichokitundika juu ya nondo kwenye dirisha la sebuleni.

Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru website yenu kwa kutupa sisi wananchi nafasi ya kutoa maoni yetu kutokana na mambo yanayotokea katika jamii yetu ya watanzani na nchi yetu kwa ujumla

MBUNGE mmoja wa Wilaya ya Kinondoni, anayedaiwa kumpiga msaidizi wake wa zamani na kumjeruhi, sasa amejulikana

WATU wanaodaiwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanatuhumiwa kuwashambulia raia katika mji mdogo wa Mbalizi, mkoani Mbeya

MKULIMA wa Kijiji cha Wendete wilayani Kahama mkoani Shinyanga Philipo Maziku (48) amekamatwa na kufikishwa mahakamani akishitakiwa kwa kosa la kumuua mwanae mwenye umri wa miaka 18 aliyemtuhumu kuiba sh. 500

Mamia ya wananchi katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameshikwa na butwaa baada ya kumuona msichana aliyedaiwa kufariki dunia takriban miaka mitatu iliyopita akiranda randa mitaani

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela msanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID' baada ya kutiwa hatiani kwa kujeruhi

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi nchini kuvamia na kufanya upekuzi katika ofisi za gazeti la MwanaHalisi na nyumbani kwa mkurugenzi wa gazeti hilo, badala ya kufanya hivyo kwa mafisadi ambao serikali imeendelea kuwalind...

RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani

Chama cha NCCR-Mageuzi, kimeitaka serikali kuutaifisha mara moja Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) unaomilikiwa na Mama Anna Mkapa.

Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi, kutumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kuwabana wanaowapa mimba wanafunzi.

Kukithiri kwa mauaji dhidi ya maalbino nchini, Mbunge wa Kuteuliwa, Bibi Al-shymaa Kwegyir (CCM), anahofia kuuawa na watu wasiojulikana,

Askofu Mkuu wa Kanisa la Sabato mkoani hapa, Joshua Kajura (63) ameibiwa gari wakati akiendesha ibada. Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Basilio Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 4 asubuhi katika kanisa lililoko huko Njiro...

Msanii Hamisi Mwinjuma a.k.a MwanaFa ama Fa anatarajia kutoka na video ya wimbo wake mpya unaoendelea kufanya vizuri katika chati mbali mbali za muziki hapa nchini unaojulikana kwa jina la ‘bado nipo nipo’ ...

Bunge limefunga rasmi mjadala kuhusu tuhuma kwamba Waziri mmoja wa zamani alionekana akifanya uchawi katika ukumbi wake. Chombo hicho cha kutunga sheria pia kimetishia kuchukua hatua kali dhidi ya magazeti na yeyote atakayeibua upya suala hilo.

Mwanamke mmoja mwenye asili ya kiarabu anatafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kupora gari aina ya Starlet aliyokodi ili limpeleke Msasani baada ya kumrubuni dereva wa gari hilo kwa sh.10,000.

Wabunge wameomba mijusi mikubwa, iliyochukuliwa nchini katika zama za wakoloni na kupelekwa Ujerumani, irudishwe nchini ili kuendeleza utalii. Baadhi ya mijusi hiyo ilikuwa na uzito mkubwa unaofikia tani 80.

Baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, jana alikuja juu akisema kwamba majina ya vigogo waliosababisha kifo cha mwanae wataanikwa hadharani...

Sakata la kikundi maarufu cha uchekeshaji nchini cha 'Ze Comedy' na Kampuni ya East Africa Televisheni (EATV), limeibukia bungeni ambapo Serikali imesisitiza kuwa kina haki ya kwenda Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...

Temeke imefunga pazia la Mkoa wa Dar es Salaam kutafuta wawakilishi wake katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2008 kwa kumuibua mtoto anayejiamini kuwa, siyo tu Miss Temeke, bali Miss Tanzania na hata Miss World 2008

Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya

Waziri wa habari na huduma ya matangazo wa Zambia Bw. Mike Mulongoti ametoa hotuba kupitia televisheni akikanusha habari kuhusu rais Levy Patrick Mwanawasa wa nchi hiyo amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kiharusi huko Paris

NAIBU Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, amesema uamuzi wa kumsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Chacha Wangwe, ni mzito na mgumu, lakini ulikuwa lazima ufanyike ili kukinusuru chama kilichokuwa kinaelekea kusambaratika

VIONGOZI wa Afrika wamelitaka kundi la mataifa manane tajiri duniani (G8) kutimiza ahadi zake za kuisaida Afrika na kuzingatia kuwa kupanda kwa bei ya mafuta na chakula kutazidisha umasikini  

  

Powered by AlphaContent Bongo5.com © 2005-2008 - All rights reserved
Total Members
total 19501 registered
female 4850 female
male 14569 male
month 98 new this month
New: carter
Who's Online Now
We have 15 guests online

Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com