Username
Password
Remember me
Lost Password?
Click here to register
Home
Friends
News
Events
Photos
Music
Videos
Forum
Games
Chat
Results 241 - 270 of 2022
Times FM kuwarusha Mashabiki Marekani
RADIO 100.5 Times FM 'Mguso wa Jamii' imeandaa droo kubwa ya safari ya siku tano ya kuwapeleka washindi watatu kutembelea Hollywood California, Marekani
Pinda ahofu mafua ya ndege nchini
SERIKALI imewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa wa mafua makali ya ndege nchini, kwa sababu ugonjwa huo kwa sasa umeshaingia Juba, kusini mwa Sudan, ambayo inapakana na Uganda na Kenya
Chenge asifia umahiri wa makachero wa Uingereza
SIKU moja baada ya wakili wake J Lewis Madorsky, kuibuka na kutema cheche, Andrew Chenge amesema makachero wa kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai kutoka Uingereza yaani Serious Fraud Office (SFO), ni mahiri na wenye mkono mrefu
Wasiwasi Bakwata
HALI ya wasiwasi wa kutokea vurugu jana ilitanda katika ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), hali iliyosababisha ofisi hizo kufungwa kwa muda
Waziri auziwa nyumba 'hewa'
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi anadaiwa kuingizwa mjini baada ya kudaiwa kununua nyumba hewa eneo la Mikocheni 'B' jijini Dar es Salaam kwa kiasi cha sh. milioni 40
Mambo ya Nje yataka kulipana posho za Sh300,000 kwa mwezi
WAKATI walimu wakiishinikiza serikali iwalipe malimbizo ya fedha wanazodai, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeanza mkakati wa kuboresha maslahi ya watumishi wake, kwa kupendekeza kuwa kila mmoja alipwe posho ya Sh300,000 kwa mwez...
|
Read more...
Mkali nani? Wanajua mashabiki
Shangwe la burudani ya kumsaka mkali wa michano ya kibongo inayoshirikisha makundi mawili ya kizazi kipya Wanaume Family na Wanaume Halisi inaendelea. Akiongea mara baada ya burudani hiyo mkoani Arusha, Meneja Masoko wa Tigo Bw Kelvin Twissa ali...
|
Read more...
Ni mpya kwenye Game…Mkali Ile mbaya
Ujio wake umeashiria ulimwengu wa muziki wa dansi kuwa kuna mashine za ukweli katika muziki huo zilizojificha na bado hazitambuliki, hasa hapa nchini kwetu Tanzania. Huyu si mwingine bali ni Blanchard De Plaizir msanii mwenye vipaji vingi..
Basi lori yagongana uso kwa uso, 4 wafariki dunia
BASI la Rafiki Trans lenye namba za usajili T 473 AMA lilokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Masasi juzi liligongana uso kwa uso na lori la mchanga lenye namba za usajili T 951 ACZ na kuua abiria wanne na kujeruhi wengine 23
Rostam sasa akimbilia mahakamani
BAADA ya kupigwa 'stop' na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwasilisha hoja yake binafsi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme kati ya kampuni hewa ya kuzalisha Umeme ya Richmond na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz (CCM...
|
Read more...
Ikulu yambana Chenge
SERIKALI imesema aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge anayetuhumiwa kumiliki dola za Marekani 1 milioni (Sh 1.2 bilioni) nje ya nchi, sasa anachunguzwa na vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa ili kubaini iwapo ana kesi ya kujibu mahak...
|
Read more...
CUF yatabiri machafuko
Chama cha Wananchi (CUF), kimetabiri Uchaguzi Mkuu wa 2010 Zanzibar kutawaliwa na maafa, ikiwa mwafaka kati ya chama hicho na CCM, hautatoa suluhisho la maelewano visiwani humo
Majambazi wampora mwingereza milioni 40/-
KATIKA kuadhimisha Sikukuu ya Muungano juzi, watu wanne walifariki dunia, huku wengine wanaoaminika kuwa majambazi walipora Sh milioni 40 katika Kampuni ya Hardison ya Mtaa wa Lindi
Kidato cha nne wafundisha sekondari
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Kahunga mkoani Kigoma, wameulalamikia uongozi wa shule hiyo kuajiri walimu waliohitimu kidato cha nne, wasiopata mafunzo ya ualimu
Robert Green Kupanda Mlima Kilimanjaro
Kipa wa kuaminika wa klabu ya Ligi Kuu ya England, West Ham, Robert Green anatarajia kushuka Tanzania akiwa na malengo ya kuja kuupanda mlima Kilimanjaro
Vimini Stooop Kanisani
Baada ya kukithiri kwa baadhi ya wadada wanaotinga na vinguo vifupi vinavyoweza kuwakwaza wengine, Kanisa la Watakatifu Mashahidi wa Uganda lililopo Magomeni Jijini limewapiga 'stop' waumini wa aina hiyo kuhudhuria ibada zake
LHRC yamtaka Waziri Mkuu kufuta Kauli yake
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) hivi karibuni kimemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuifuta kauli yake ya kuwa Serikali inashindwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watuhumiwa wa ufisadi waliojichotea mabilioni ya shilingi
36 wafukuzwa Chuo Kikuu
Serikali imewafukuza chuoni wanafunzi 36 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani waliohusika katika vurugu zilizotokea chuoni hapo juzi usiku na kusababisha askari polisi wawili kujeruhiwa miguu
Amuua Mtoto kwa kumnywesha sumu ya panya
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwakibete mkoani Mbeya aliyejulikana kwa jina la Bibi Sikujua John (31) anashikiliwa na Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuua mwanawe kwa kumnywesha sumu ya panya
Wanazuoni watumie Lugha ya Kiswahili - Mkuchika
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amewaonya wanazuoni mahiri wa lugha ya Kiswahili na maprofesa kwamba, iwapo lugha za Kiafrika hazitaandikwa zitakuwa katika hatari ya kufa
Tatiana atua Dar
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa 2, Tatiana Durao, kutoka Angola, amewasili nchini leo, kwa ajili ya maonyesho mawili ya mavazi yatakayofanyika Aprili 25, jijini Arusha na kesho yake jijini Dar es Salaam
Msaidizi wa Chenge atoa kali
Naibu Waziri wa Miundombinu Dokta Makongoro Mahanga ametoa kali Bungeni baada ya kusema anajibu swali kwa niaba ya Waziri katika wizara hiyo ambaye ameshaachia ngazi
TANESCO inaendeshwa kwa hasara
IMEBAINIKA kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekuwa likiendeshwa kwa hasara ya kati ya sh bilioni 107 na bilioni 189 kila mwaka tangu mwaka 2004 hadi kufikia mwaka 2007
Rais mstaafu Mkapa, mkewe waumbuliwa bungeni
MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), amewatuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe Mama Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kuwa walinunua mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, kwa kificho
Chenge abwaga manyanga
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Ikulu, jijini Dar es Salaam jana usiku na kukaririwa na Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) na baadhi ya vyombo vingine vya habari, Bw. Chenge alimwandikia barua ya kujiuzulu Rais Jakaya Kikwete jana.
Ditopile afariki dunia
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni mstaafu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia katika Hoteli ya Hilux, iliyopo mkoani Morogoro
Kuwasaidia watu wengine ni njia ya kumshukuru Mungu-Mengi
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi amesema ushirikiano katika kuisaidia jamii hususani watu maskini wasio na uwezo, ni jambo la heshima kwa binadamu na njia bora ya kuuthamini utu wa mwanadamu
Sumatra kuwashughulikia wanaopandisha nauli
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imeomba msaada wa polisi, ili kuwadhibiti makondakta wa daladala wanaopandisha nauli kiholela
Raza aponda kura ya maoni
Mfanyabiashara maarufu wa visiwani Zanzibar, Bw. Mohammed Raza, ameyaponda maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) ya kutaka kuitisha kura ya maoni juu ya serikali ya mseto
JK awakutanisha viongozi kuijadili Zimbabwe
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, amekutana na viongozi mbalimbali duniani kujadili masuala makubwa likiwepo la Zimbabwe na kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais
<< Start
< Prev
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next >
End >>
[ Back ]
Top
Powered by
AlphaContent
Bongo5.com
© 2005-2008 - All rights reserved
Total Members
19501 registered
4850 female
14569 male
98 new this month
New:
carter
Who's Online Now
We have 20 guests online and 1 member online
nataone
Total of members in the chatroom:
Home
|
Search
|
Contact Us
|
Sitemap
2006-2007 © Copyright Bongo5.com